VIONGOZI wa Chama
cha Wamachinga Kariakoo (KAWASO), wamesema wataendelea kupigania changamoto za
wamachinga wa Kariakoo na Tanzania kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Mweneyekiti wa Kawaso, Stephen Lusinde alipofanya mahojiano makao makuu ya Kawaso Kariakoo Dar es Salaam.
“Ninamshukuru Mungu mimi binafsi
na kwa niaba ya viongozi wenzangu, wajumbe, na wanachama wote walioturudisha
madarakani na hata ambao hawakutuchagua tutawatumikia pasipo ubaguzi wowote kwani
wito wetu ni kuwatumikia wamachanga” alisema Lusinde
Aidha Lusinde amewataka
wamachinga kuendelea kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano na wasisite kuona
uongozi pale zinapotokea changamoto kwakuwa wapo kwa ajili ya kuwatumikia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti
wa Kawaso, Yusuphu Namoto amesema haikuwa rahisi kushinda uchaguzi huo
kutokanana na mizengwe ya hapa na pale lakini walimuachia Mungu ili achukuwe
nafasi yake katika jambo hilo adhimu na muhimu katika Maisha yao kama
wafanyabiashara.
“Ifahamike kwamba tokea
kuanzishwa kwa Kawaso tokea 2017 hakujawahi kufanyika uchaguzi wowote na huu
ndiyo uchaguzi wa kwanza kufanyika na wanamshukuru Mungu na wapiga kura kwa
kuwaamini na kuwarejesha madarakani” alisema Namoto
Akizungumzia siri ya ushindi wao
alisema ni kujituma katika katika kuwatumikia wamachinga hususani utatuzi wa
changamoto zinazowakabili kadri ya uwezo wao.
Uchaguzi huo ulifanyika April 26,
2024, ambapo Stephen Lusinde amerejeshwa katika nafasi yake ya Uenyekiti,
Namoto akiwa Makamu Mwenyekit, na Katibu ni Borno Nanyimbura, Naibu Katibu ni
Sabiti Maloua, Mhazini Ally Haji, Agostino Choga.
No comments:
Post a Comment