USAFIRI WA MABASI UMEANZA KUTOKA AFRIKA KUSINI HADI TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 24 August 2023

USAFIRI WA MABASI UMEANZA KUTOKA AFRIKA KUSINI HADI TANZANIA



HII ni habari njema kwa wasafiri kwenda Afrika Kusini na kurudi. Kwa sasa Watanzania wanaweza kusafiri kwa raha kwa basi kutoka Dar-Es-Salaam hadi Johannesburg, Afrika Kusini na kampuni ya kizalendo ya 'Mkombe Luxury Bus ambayo ina makao yake Johannesburg Afrika kusini. Kwa sasa wasafiri wa Tanzania na Afrika Kusini wanaweza kutumia usafiri huo wa Mkombe Luxury Bus kusafirisha pia mzigo. Nauli ya mtu mmoja ni Tsh 350,000 za kitanzania kwa safari moja na unaweza kulipia nauli ya Tsh,700,000 kwenda na kurudi pia.

Kampuni ya Mkombe Luxury Bus imefungua ofisi zake Mtaa wa Shekilango jijini Dar-es-Salaam ambapo tiketi zinapatikana muda wote ofisini. Pia mteja anaweza kupata tiketi kwa whats app +27604749717. Wasafiri wa Tanzania na South Africa wanaweza kutumia usafiri huu unao pitia Zambia, Maporomoko ya maji ya Victoria Falls, Zimbabwe hadi Johannesburg Afrika Kusini. 

Safari nzima huchukua siku tatu hadi Afrika kusini, Kampuni pia inamagari ya kusafirisha mizigo. Safiri kwa Raha na Mkombe Luxury Bus na Usafiri kitalii zaidi.

No comments:

Post a Comment