![]() |
Adeladius Makwega-DODOMA
Wakristo wameambiwa kuwa lazima
wawe na kiu ya kumuona Mwenyezi Mungu, maana katika ulimwengu wa sasa watu
wanakiu na mambo ya kidunia mathalani kusoma ujumbe wa whasaap lakini haya
hayasaidii chochote katika kumuona Mungu .
Mtu akiamka tu anakimbilia
kuangalia kwenye simu yake kuna nini? Je wewe muumini una kiu ya kusoma neno la
Mungu?
“Wale
Wayunani walikuwa na kiu ya kumuona Kristo, walikuwa na kiu ya kumuona Mungu.
Je Wakristo tuna kiu ya kumuona Mwenyezi Mungu?Je tunakuja kanisani na nia ya
kumuona Mungu? Je umuone katika njia gani? Umuone katika sakramenti, Sakramenti
gani? Sakramenti ya kumrudia Mwenyezi Mungu.
Sisi
kama wakristo lazima tuwe na kiu ya kumuona Mwenyezi Mungu, katika hizo Sakramenti
zake Sakrament ya Ekaristi Takatifu, Sakramenti ya Kitubio na Sakramenti ya
Ndoa.”
Haya yamesemwa na Padri Kenneth
Ogoti katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata- Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo
Kuu Katoliki la Dodoma katika misa ya kwanza ya dominika ya 5 ya Kwaresma ya Mwaka
B wa Liturjia ya Kanisa.
Padri Ogoti akihubiri katka
misa ya kwanza ya Jumapili ya Machi 17, 2024 iliyoanza saa 12. 30 ya asubuhi
alisisitiza kila muumini kuwa kiu hii ya kumuona Mungu.
Mahubiri haya yalihitimishwa
kwa Padri Ogoti ambaye anahudmu katika shule mojawapo ya sekondari ya jimbo
hili akinadi kuwa mtu anayeipeda nafsi yake ataipoteza, tusijipende kupita
kiasi.
Misa hiyo pia iliambatana na
nia na maombi kadhaa,
“Utujalie
kukubali na kupokea mabadiliko ya maisha yetu- Eee Bwana-Twakuomba Utusikie.”
Wakati wa kupokea waaamini
walijongea mbele altare huku baadhi yao walijongea katikati ya kanisa hilo,
mbele akiwa Frateri na katikati akiwa Padri Ogoti wakikomunisha
Wakati wa zoezi hilo jirani
na alipokuwapo Padri Ogoti muumini mmoja kwa bahati mbaya alipopokea Ekaristi iimponyoka,
mara moja Padri Ogoti aliikota na muumini huyu kukomunika, kumbuka ndani ya umbo
la mkate ni Yesu mwenyewe.
Hadi misa hiyo inakamilika
majra ya saa mbili ya asubuhi, hali ya hewa ya Chamwino Ikulu ni jua la kadli kwa
juma zima.


No comments:
Post a Comment