MKANDARASI BARABARA YA MZUNGUKO WA NJE DODOMA AHIMIZWA KUZINGATIA MKATABA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 18 March 2024

MKANDARASI BARABARA YA MZUNGUKO WA NJE DODOMA AHIMIZWA KUZINGATIA MKATABA

 

Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa barabara ya Mzunguko wa Nje (Dodoma City Outer Dual Carriageway Ring Road) unaoendelea jijini Dodoma


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje jijini Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) sehemu ya Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala yenye urefu wa kilometa 60 ambao ujenzi wake umefikia asilimia 60.31 alipotembelea na kukagua mradi huo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour (wa tatu kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje jijini Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) sehemu ya Nala-Veyula-Mtumba-Ihumwa yenye urefu wa kilometa 52.3 ambao ujenzi wake umefikia asilimia 74.46 unaotekelezwa na Mkandarasi Inter-Consult

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi, Aisha Amour amemwagiza mkandarasi anayejenga barabara ya mzungumzo jijini Dodoma kufanya kazi kwa mujibu wa mkataba, kutekeleza maagizo anayopewa na viongozi wakati wa ukaguzi wa miradi.

Alitoa maagizo hayo leo jijini Dodoma wakati akikagua mradi wa ujenzi huo kwa kiwango cha lami wenye urefu wa km 112.3 sehemu ya Barabara ya Ihumwa Dry Port- Matumbulu - Nala yenye urefu wa km 60.


Pamoja na mambo mengine, Balozi Aisha alimtaka Mkandarasi huyo  kuhakikisha anazingatia ubora wa kila tabaka kabla ya kuendelea na tabaka lingine, kupima mali ghafi za ujenzi, kuhakikisha ubora kabla ya kuzitumia ili kuzuia barabara hiyo kuharibika kabla ya wakati.


“Hakikisheni mnatumia maabara vema na mkandarasi ahakikishe vifaa vyote vya maabara vinakuwa eneo la ujenzi kipindi chote cha utekelezaji wa mradi” alisema Balozi Aisha.


Pia, aliwataka kuhakikisha wanapambanua mapungufu hayo na kuweka mkakati wa kuyafanyia kazi kwa wakati ili kuleta matokeo chanya.


Aidha, amewataka kufanya kazi kwa kizingatia misingi, kanuni na sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa maeneo ya kazi.


“Hakikisheni wafanyakazi hawajiingizi katika vitendo vya rushwa kwa kupunguza mianya ya rushwa nyakati zote wakati mradi unatelelezwa” alisisitiza Balozi Aisha.


Mradi wa mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma wenye urefu wa km 112. umegawanywa katika sehemu mbili za utekelezaji ukijumuisha
Sehemu ya kwanza ya Nala - Nyeyula - Mtumba - Ihumwa Dry Port (km 52.3) ambapo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 76 na
Sehemu ya pili ya Ihumwa Dry Port- Matumbulu - Nala (km 60) ambapo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 60. 

No comments:

Post a Comment