![]() |
| Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) kuongeza |
Waziri wa Ujenzi, Innocent
Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) kuongeza wigo wa
kuwajengea uwezo Wahandisi Washauri nchini ili kuhakikisha utalaam na ujuzi
unakuzwa kwa maendeleo ya nchi.
Bashungwa amezungumza hayo
jijini Dodoma katika mkutano uliokutanisha Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya
Usajili ya Wahandisi (ERB), na kusisitiza kuweka mikakati mahususi ya
uendelezaji wa Wahandisi Washauri kitaaluma ili kukuza tasnia ya Uhandisi.
“Vipaumbele na maagizo ya
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
katika sekta hii ni kuona ushiriki mkubwa wa Wahandisi na Makandarasi Wazawa
katika kazi za ujenzi na usimamizi wa miradi (Local Content), sisi kama
wasaidizi wake tuhakikishe tunalitekeleza hili”, amesema Bashungwa.
Aidha, ameelekeza
kuhakikisha kunakuwa na uwepo wa ushirikishwaji wa Wahandisi wahitimu katika
mpango wa mafunzo kwa vitendo (SEAP) kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa
nchini ili kuwajengea uwezo.
Vilevile, ameagiza
kuangalia maeneo yote yenye changamoto katika Sheria ya Usajili ili kuwawezesha
wahandisi kufanya ubunifu na kusaidia nchi katika uchumi wa viwanda na
maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
“Tengenezeni mazingira
wezeshi kwa Wahandisi Washauri wazawa kuweza kushiriki katika miradi ili kuokoa
fedha za Serikali”, ameagiza Bashungwa.
Kwa upande wake, Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Eng. Aisha Amour, ameishauri Bodi na Manejimenti ya
ERB kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi kazini.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Eng. Menye Manga, ameahidi
kushirikiana na Menejimenti ili kuleta mabadiliko chanya katika Taaluma ya
kihandisi na kuhakikisha taaluma inaendelezwa na kukuzwa ili kuongeza idadi ya wataalam
hao nchini.


No comments:
Post a Comment