Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amepokea nakala za hati za
utambulisho za Balozi Mteule wa Libya
nchini, Mhe. Abulmajed Albhloul Alshatewi katika hafla fupi
iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Makamba amemkaribisha nchini Mhe.
Alshatewi na kumuahidi ushirikiano wa Wizara na Serikali kwa ujumla wakati wote atakaokuwa akitekeleza majukumu yake nchini.
Aidha, Waziri Makamba ameongeza kuwa ushirikiano
kati ya Tanzania na Libya umedumu kwa zaidi ya
miaka 50 na na wakati wote umekuwa imara. “Tunaamini kuwa Mhe. Balozi wakati wa
uwakilishi wako uhusiano baina ya mataifa yetu utaendelea kuimarika zaidi
katika sekta mbalimbali za kimkakati,” aliongeza Waziri Makamba.
Kwa upnade
wake Balozi Mteule, wa Libya nchini, Mhe. Abulmajed Albhloul
Alshatewi amesema kuwa atafanya kazi kwa ushirikiano
na Tanzania wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi hapa
nchini.
Ni faraja
kwangu kuja kufanya kazi Tanzania naahidi wakati wote wa uwakilishi wangu hapa
Tanzania kama Balozi tutafanya kazi kwa ushirikiano katika kunendeleza sekta
mbalimbali hususan biashara na uwekezaji, kilimo na nyingine.
Katika
tukio jingine, Waziri Makamba amekutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Uswisi
nchini, Mhe. Didier Chassot, Balozi wa Vatican nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo
Accattino pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini, Bw. Robert Raines.
Pamoja na
mambo mengine, Waziri Makamba amejadiliana na Mabalozi hao masuala mbalimbali
ya ushirikiano wa uwili, kikanda na ushirikiano wa kimataifa baina ya Tanzania
na nchi zao.
.jpg)
.jpg)

No comments:
Post a Comment