Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza
wakati wa Mkutano wa 11 wa Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania (Tanzania
Women CEOs Roundtable) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati akifungua rasmi Mkutano
wa 11 wa Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania (Tanzania Women CEOs
Roundtable) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa
Jukwaa la Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania (TWCR), Bi. Emma Kawawa
akieleza jambo wakati wa Mkutano wa 11 wa Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake
Tanzania (Tanzania Women CEOs Roundtable) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa 11 wa Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania (Tanzania Women CEOs Roundtable) uliofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana wa kike na wanawake nchini kuchangamkia fursa zilizopo ili kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Katambi ameyasema hayo
wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa
Mkutano wa 11 wa Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania uliofanyika jijini
Dar es Salaam.
“Wanawake ni jeshi kubwa na
Serikali ina matarajio makubwa na kundi hilo katika kuweza kushiriki vema
kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi yetu na jamii kwa ujumla,” amesema.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali
inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa rasilimali
watu ni nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
Halikadhalika, Naibu Waziri
Katambi amewasilisha maagizo ya Waziri Mkuu kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanzania
Women CEOs Roundtable ambapo ameitaka TWCR kushirikiana na Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC) ili kubaini maeneo yenye uhitaji na kuandaa programu za kujenga
uwezo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto na Makundi Maalum
iimarishe kanzidata ya Viongozi na Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake katika
Sekta ya Umma pamoja na Sekta Binafsi.
Vilevile, Bodi hiyo na Taasisi za
Sekta Binafsi ziangalie namna ya kujenga uwezo kwa wataalam wabobezi wanawake
katika uendeshaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya Kitaifa, kutengeneza
mikakati itakayoleta matokeo chanya katika ustawi wa wanawake na Taifa kwa
ujumla, imarisheni huduma za uwezeshaji katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja
na makundi ili kupunguza umaskini na Utoaji na tuzo na vyeti kwa Maafisa
Watendaji Wakuu Wanawake wanaofanya vizuri kwenye Taasisi na sekta mbalimbali
ni jambo la msingi katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake wengi kwenye
shughuli za kuchumi nchini.
Kwa upande wake, Mwanzilishi na
Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Maafisa Watendaji Wakuu Wanawake Tanzania (TWCR),
Bi. Emma Kawawa ametoa wito kwa wanawake kuwa wajasiri, kujiamini na kuthubutu
katika kuanzisha Biashara ili kujikomboa kiuchumi.
.jpg)
.jpg)



No comments:
Post a Comment