RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI BARABARA RUANGWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 18 September 2023

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI BARABARA RUANGWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa na viongozi wengi akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Nachingwea – Ruangwa, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (km 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Lindi, Septemba 18, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Nandagala mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Nachingwea – Ruangwa, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (km 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, Septemba 18, 2023, mkoani Lindi.

Muonekano wa sehemu ya ujenzi wa barabara ya Nachingwea – Ruangwa, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (km 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Lindi ambapo  Septemba 18, 2023, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili kijiji cha Nandagala kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Nachingwea – Ruangwa, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (km 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Lindi, Septemba 18. 2023.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Nachingwea – Ruangwa - Nanganga, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (km 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, leo tarehe 18 Septemba 2023.


Akizindua ujenzi wa barabara hiyo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kujenga miundombinu ya mikoa ya kusini ili kurahisisha usafirshaji wa mazao na kukuza uchumi wa mikoa hiyo na kuwataka wakandarasi wakamilishe ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati.


"Niwaombe wakandarasi na wasimamizi waende kwa kasi sana lakini nipongeze TANROADS mkandarasi na wengine kwa hatua ambayo imeshafikia na kwetu sisi Serikali mafedha yapo tunasubiri certificate [cheti] ziletwe tulipe kazi ziendelee"- amesema Rais Dkt. Samia.


Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema lengo la Serikali ni kuunganisha mkoa wote wa Lindi kwa kiwango cha Lami na wilaya kwa wilaya ziunganike kwa lami.


"Niwaombe mpokee maendeleo yanayokuja tufanyaje kazi kwa pamoja langu kubwa la kuwaomba maendeleo ni fedha ndugu zangu na fedha inapatikana tunapouza bidhaa na nyinyi ni wakulima wazuri wa Ufuta, Mbaazi na Koroshop na bei ya ufuta na mbaazi mmeiona mwaka huu, tunafanya kazi tuone korosho nayo iwe na bei nzuri"- amesisitiza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa barabara hiyo mbele ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta, amesema mkandarasi anayejenga barabara hiyo ni China 15th Group kwa thamani ya Shilingi Bilioni 50.3 na jumla ya Shilingi Bilioni 1.1 ikiwa ni sehemu ya Ongezeko la Thamani na kutumika kulipa fidia ya mali na ardhi kwa watu walioathirika na ujenzi kwa mujibu wa Sheria.


"Mheshimiwa Rais ujenzi wa Barabara unasimamiwa na TECU ambacho ni kitengo cha TANROADS na maendeleo ya ujenzi mpaka sasa tumefikia asilimia 71, na mapaka sasa tumeshalipa jumla ya shilingi Bilioni 20.7 na zilizobaki tunaendelea kulipa kwa utaratibu uliowekwa"- Amesema Mhandisi Besta.

No comments:

Post a Comment