RAIS SAMIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KUELEKEA KWENYE KILELE CHA TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 29 August 2023

RAIS SAMIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KUELEKEA KWENYE KILELE CHA TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akiangalia michoro ya viwanja vya kufurahisha Watoto Kizimkazi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la Kisasa la Kizimkazi Dimbani kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Watendaji wengine wakishuhudia.

Wananchi wa Kizimkazi wakiwa nje ya Kituo cha Afya Kizimkazi Dimbani katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui wakati akizindua ugawaji wa gari la Wagonjwa kwa ajili ya Kituo cha Afya Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Kituo cha Afya cha mama na mtoto Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua ugawaji wa Gari la OCD Kizimkazi Mkunguni pamoja na Gari la OCD Makunduchi tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe ufunguzi wa Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B (Muyuni Community Hall) kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B (Muyuni Community Hall) kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akikagua Madarasa ya Shule ya Msingi Muyuni B mara baada ya ufunguzi katika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akivuta kitambaa kufungua Madarasa 6 ya jengo la Skuli ya Msingi Muyuni B tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

No comments:

Post a Comment