Sehemu ya washindi wa pikipiki 11 zenye thamani ya shilingi millioni 33 zilizotolewa na NMB wakifurahiya zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa. |
Baadhi ya washindi wa pikipiki 11 zenye thamani ya shilingi millioni 33 zilizotolewa na NMB wakifurahiya zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa. |
Na Mwandishi Wetu, Dar
JUMLA ya Washindi 200 katika shindano la ‘Bonge la Mpango’ msimu wa Tatu lililokuwa likiendeshwa na Benki ya NMB ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha wananchi hasa wateja wa NMB kujiwekea akiba ameibuka washindi na zawadi mbalimbali zikiwemo bajaji za mizigo tano zenye thamani ya milioni 25, pikipiki 11 zenye thamani ya milioni 33, friji la kisasa la milango miwili.
Leo katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam yanapoendelea Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa ndani ya Banda la Benki ya NMB washindi 22 wengine wamekabidhiwa zawadi zao mara baada ya kuibuka washindi.
Akikabidhi zawadi hizo, Mkuu wa Mtandao wa Matawi na Mauzo ya Rejareja wa Benki ya NMB, Bw. Donatus Richard amesema washindi hao wanakamilisha jumla ya washindi 200 waliojinyakulia zawadi anuai katika shindano hilo la Benki ya NMB iliyopewa jina la ‘Bonge la Mpango’ Msimu wa Tatu.
Bw. Richard alisema shindano hilo limekuwa na mafanikio makubwa na kuvutia wananchi ambapo jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 180 zimenyakuliwa na wateja baada ya kuibuka washindi katika droo mbalimbali zilizoendeshwa.
"...Niseme kwa ujumla imekuwa ni promosheni nzuri ambayo tumeihitimisha leo, lakini niendelee kuwaasa Watanzania popote walipo wanapofikiria kupata suluhisho la huduma za kibenki waifikirie Benki ya NMB kwa sababu ipo kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania kwa masharti nafuu na rafiki huku ikijali zaidi matakwa ya Watanzania.
Naweza nikatoa mfano mmoja tu ukiwa na akaunti ya NMB moja ya moja kati ya faida kubwa unapata kwanza tunaunganisha simu yako na akaunti yaani NMB Mkononi kwenye NMB mkononi kuna manufaa mengi unapata moja niseme ukiwa nayo unapata unapata mkopo tunaita 'mshiko fasta' kwenye mkopo huu mtu unaweza kukopa kuanzia 1000 hadi laki tano (500,000/=) kwa muda wowote ambao mteja anahitaji bila masharti yoyote wala kwenda benki," alisema Mkuu huyo wa Mtandao wa Matawi na Mauzo ya Rejareja wa Benki ya NMB, Bw. Richard.
Aidha alizitaja zawadi zilizoshindwa kuwa ni pamoja na bajaji za mizigo tano zenye thamani ya shilingi millioni 25, pikipiki 11 zenye thamani ya shilingi millioni 33, friji (jokofu) la kisasa la milango miwili, Smart Tv, mashine ya kufulia nguo, Laptop, simu ya Samsung Z Flip pamoja na simu ya iphone 14 ProMax.
No comments:
Post a Comment