Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai (ProLife Tanzania) Emil Hagamu (pichani mbele) akitoa elimu katika semina zake kwa jamii. |
Na Frida Manga, Dar Es Salaam
KASI ya kuwepo kwa ndoa za jinsia moja kunaweza kufananishwa na Kisa cha Mfalme Farao kutaka kumuua Mtoto Yesu na kuagiza kuuawa kwa watoto wa kiume kipindi kile cha kuzaliwa kwa Masiha.
Hii ni kwa sababu, muunganiko wa ndoa ya jinsia moja, yaani mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke siyo mpango wa uumbaji wa Mungu ambaye ni asili ya Uhai mpya alioutengeneza kati ya mtu mke na mtu mume ambapo kupitia wao unapatikana Uzao.
Ndoa ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke, walioamua kwa ridhaa yao wenyewe kuishi pamoja mke na mume mpaka mwisho wa uhai wao kadiri ya mpango wa Mungu.
Ndoa za jinsia moja ama Ushoga ni ushetani wenye mkakati wa kaifanya Dunia kuwa jangwa lisilo na uzao wa binadamu kwani ni kinyume na Mpango wa Mungu wa uumbaji wa Mwanadamu.
Katika moja ya kauli zake, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai (ProLife Tanzania) Emil Hagamu anasema ni batili na kufuru kwa watu wa jinsi moja kuoana(kufunga ndoa). Na kiukweli hiyo haina hadhi ya kuitwa ndoa bali ni uchafu baina ya hao wanaoshiriki.
"Mungu hakutupatia ujinsia kwa ajili hiyo, kama anavyosema katika neno lake, (Mwa.1:26-28; 2:20-25), Upendo wa kindoa unabubujika kwa uasili wake kutoka kwa mtu mume kwenda kwa mtu mke, na ina sifa siyo tu ya kuleta uzao bali uzao wa watoto wengi, (Mwa.1:28, 2:23, 4:1-2, Zab.128:3-4)" Alisema Hagamu.
Alisema ushiriki wa jinsia moja ni itikadi inayokataa uzazi na uzao, na badala yake wanasayansi wenye mlengo huo wanatengeneza madodoki na kujihusisha nayo kimapenzi (sexual doles).
Ni itikadi inayoshinikizwa na baadhi ya watu mashuhuri na wenye fedha kutoka nchi za Magharibi ambao wamepoteza kabisa utambulisho wao kibinadamu, itikadi ambayo inaenea duniani kwa nguvu ya fedha na katika nchi mbalimbali zinazoendelea kwa kuweka vitisho, vikwazo na masharti katika mikopo ya fedha na misaada ya kimaendeleo,
Hagamu anasema kwa kutumia udhaifu wa baadhi ya viongozi wa dini na baada ya kupuuzia mafundisho ya kweli ya dini, itikadi hiyo imeota mizizi katika taasisi za dini na baada ya kupata ridhaa, itikadi hiyo sasa inaenea duniani kote pasipo kizuizi chochote kile.
Kwa kuzingatia umuhimu wa uhai na familia; Shirika la kutetea Uhai Prolife limeunda mtandao wa waandishi wa habari za uhai na familia; Tanzania Journalists for Life and Family Network {JOLIFATZ}ambao Mwenyekiti wake ni ndugu Gaudence Hyera anayefanya Utume wake katika Kituo cha Tumaini Media, Dar Es Salaam.
Miongoni mwa malengo ya JOLIFA TZ ni Kubuni, kuandaa na kutekeleza Kampeni kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Binadamu kwa kuheshimu Tunu halisi za Utamaduni wa kiafrika na kulinda thamani ya Uhai wa Binadamu kwa kupinga mitazamo na matendo yanayodhalilisha na kuharibu Utu wa binadamu.
Mtandao huo haubagui Dini, Dhehebu wala rangi unajumuisha wanachama kutoka vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii hapa nchini na umeshajiunga na mtandao wa waandishi wa habari za uhai na familia kwa nchi zinazozungumza lugha ya kiingereza katika Bara la Afrika.
Baadhi ya nchi hizo ni
Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Afrika Kusini, Nigeria…. ambao hivi karibuni
walifanya Mkutano kwa njia ya Video kujadili changamoto zinazosababisha vikwazo
katika kupambana na kampeni potofu dhidi ya Uhai na familia.
No comments:
Post a Comment