MTENDAJI MKUU UCSAF AVUTIWA NA USHIRIKIANO WA TTCL SABASABA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 8 July 2023

MTENDAJI MKUU UCSAF AVUTIWA NA USHIRIKIANO WA TTCL SABASABA

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi.Justina Mashiba (kulia) akipokea zawadi mara baada ya kutembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifaya Sabasaba 2023 jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi.Justina Mashiba akipata maelezo mbalimbali ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifaya Sabasaba 2023 jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi.Justina Mashiba (wa pili kulia) akipata maelezo mbalimbali ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifaya Sabasaba 2023 jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi.Justina Mashiba (kulia) akiuliza jambo ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifaya Sabasaba 2023 jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi. Justina Mashiba (katikati) akipata picha ya kumbukumbu na maofiza wa TTCL ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifaya Sabasaba 2023 jijini Dar es Salaam.

MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Bi.Justina Mashiba ametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL katika Maonesho ya Sabasaba 2023.

Akiwa katika banda hilo Bi.Justina amesema, TTCL na UCSAF wamekuwa na mahusiano mazuri ambayo yamewezesha kufanikisha huduma mbalimbali kwa wananchi zinazotolewa na pande zote mbili za taasisi yaani TTCL na UCSAF. 

Aidha Bi.Justina ameahidi kuendelea kufanya maboresho zaidi ya kiushirikiano hali ambayo itawezesha kufanya vizuri katika maonesho ya Sabasaba mwakani. 

Kwa mwaka huu huduma ya utoaji wa Free Wi-Fi ndani ya Viwanja vya Sabasaba wananchi wamenufaika na huduma hiyo kwa maeneo zaidi ya 17 yenye mikusanyiko ya watu yamekuwa yanapata huduma hiyo kwa ushirikiano wao.

#TTCLKivinginezaidi 

#TanzaniaMahaliSahihipaBiasharanaUwekezaji 

#OpeningthedoorstodigitalTanzania

No comments:

Post a Comment