CHUO Kikuu Mzumbe kimebuni mfumo wa Kidigitali wa kutuza kumbukumbu za wagonjwa waliolazwa Hospitalini.
Ikiwa mfumo huu utatumika basi utakwenda kuondoa mifumo ya utuzaji kumbukumbu za wagonjwa waliolazwa ambapo awali zilikuwa zikitunzwa kwenye makaratasi.
Akizungumza katika Viwanja vya Maonyesho 47 ya Biashara ya Kitamaifa jijini Dar es Salaam, Mwanafuzi wa Kitivo cha Sayansi na Teknolojia kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Frank Msonge alisema chuo kimejidhatiti katika tafiti za kuhakikisha kwamba mifumo ya Hospitali inaendelea kuwa ya Kidigitali kutokana na Maendeleo ya Teknolojia.
"Kauli Mbiu ya
Maonyesho ya mwaka huu ni, Tanzania ni Mahala sahihi pa uwekezaji Pamoja na
Biashara, imelazimu Chuo kwendana na Ujumbe wa Kauli Mbiu hiyo, Alisema.
Kwa mujibu wa Msonge mfumo huo si mpya bali ni mfumo ambao utakwenda kuboresha zaidi kuungana na mifumo iliyoko hospitalini na kuongeza ufanisi katika kupata taarifa za mgonjwa na kuepuka usumbufu wa kupotea kwa taarifa.
Msonge ameeleza namna utakavyofanya kazi kuwa, daktari atategenezewa taarifa za Kielectronic kupitia simu yake ya kiganjani (Mobile Application) ambapo atapata taarifa zote za Mgonjwa kutoka moja kwa kwenye Database ya Hospitali.
Alisema Kifaa hicho kinachajiwa na kinauwezo wa Kukaa na chaji kwa muda siku 14 bila kuishiwa chaji na kinaweza kutumika katika maeneo ya vijijini hata katika maeneo ambayo hayana Mtandao wa Internet.
Alisema kwa sasa wanaendelea kukamilisha utendaji kazi wa mfumo huo na kukamilika na kupata maoni ya Wadau utawasilishwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kuufanyia kazi.
Alisema wao kama Watafiti na Wabunifu ni kuhakikisha wanatatua matatizo yaliyoko kwenye jamii nakuona Tafiti hizo zinatumika na kuleta mabadiliko katika jamii.


No comments:
Post a Comment