Na Faustine Gimu, Sengerema-Mwanza
JAMII imetakiwa
kubadili tabia na kuona kuwa wanawake kuambatana na wenza wao vituo vya kutolea
huduma za Afya ni jambo la kawaida.
Hayo yameibainishwa katika
kijiji cha Ilekanilo, Kata ya Kasungamile Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza
baada ya timu iliyonufaika na Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii
(Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa
na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za
Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID Uzazi
Staha kufika katika kijiji hicho na kushirikisha jamii namna huduma za
afya zinavyotolewa.
Akizungumza katika
kijiji cha Ilekanilo ikiwa ni utekelezaji wa Mafunzo ya Tathmini Shirikishi
ya Kijamii (Community Score Card) kupitia mpango wa Huduma za Afya ya Jamii, Mratibu
wa Uhamasishaji na Uelimishaji Elimu ya Afya ngazi ya Jamii (DCBHPco) Wilaya
ya Sengerema Rachel Ntogwisangu amesema asilimia kubwa wanaume wa
Sengerema wamekuwa wakikwepa kuambatana na wake zao vituo vya kutolea huduma za
afya hasa kipindi cha ujauzito wakikwepa kuchekwa na jamii iwapo hawajawatunza
hivyo amesema ni muhimu wenzi wote wawili kubadili tabia na kuongozana kwenda
kliniki.
“Mjamzito ni muhimu
sana kwenda kupata huduma za afya akiambatana na mmewe, hii itasaidia
kushauriana kwa pamoja namna ya kupanga uzazi na malezi sahihi na ushauri wa
watalaam wa afya kwa pamoja hata kama kuna viashiria vya maambukizi upataji wa
huduma sahihi kwa wote ni rahisi “amesema
Kwa upande wake Diwani
wa Kata ya Kasungamile Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Godfrey Joseph
ambaye alikuwa mwenyekiti katika mkutano huo shirikishi kwa jamii kuhusu huduma
za Afya ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuja na Mpango huo Shirikishi hali
itakayosaidia wananchi kubadili tabia na kuwa na matokeo chanya.
“Tumekuja kupata elimu
ya pamoja hii itasaidia baada ya siku chache mambo yatakwenda vizuri,tunaishukuru
sana Wizara ya Afya kwa kuja na Mpango shirikishi na tuendelee kushirikiana kwa
ujumla katika uboreshaji wa huduma na tumeshirikishwa kwa kuulizwa maswali je, tunapokeaji
huduma na si kwa ugomvi ni namna nzuri tu ya kurekebisha kasoro ndogondogo ili
sote twende pamoja” amesema.
Afisa Program
huduma za afya ngazi ya jamii, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya
Kinga, Wizara ya Afya Orsolina Tolage amesema Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais,
TAMISEMI pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuhakikisha jamii
inakuwa na mabadiliko chanya katika masuala ya Afya na kuwataka vijana kuwa
mstari wa mbele kwa masuala hayo.
"'Jukumu la Wizara ya Afya kuendelea kutoa Miongozo, kusimamia na kufanya
ufuatiliaji" amesema.
Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [OR-TAMISEMI] Martha Mariki akisema wataendelea kusimamia sera
katika kuhakikisha huduma za Afya zinaimarishwa ngazi ya Jamii
Mratibu wa Uhusiano
Jamii na Mabadiliko ya Tabia kutoka Americares Mussa Lunyonga amesema hatua
hiyo ya Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) kupitia
Wizara ya Afya, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES
na TAMISEMI imekuwa na chachu kubwa kwa wananchi kueleza namna wanavyopokea
huduma za afya na kurahisisha namna ya kuweka mikakati ya pamoja katika
uboreshaji.
Nao baadhi ya Wananchi
wa kijiji cha Ilekanilo akiwemo Bugumbi Mwarabu, Jackson Mletwa, Yubi
Busenga pamoja na Lucas Petrol wamesema Mafunzo shirikishi yamesaidia
kuwabadili tabia hususan Elimu ya Afya ya Uzazi huku wakizungumzia chanzo
kinachosabisha vijana wa kike kwenda vituo vya kutolea huduma za Adfya peke yao
bila wenzi.
“Unakuta kijana wa kike amekutana na waume wanne watano, inapofika
muda anashindwa hiyo mimba anampa nani hivyo hivyo kijana wa kiume naye unakuta
ana wasichana sita matokeo yake ni kukataa mimba, matokeo yake anafika kwenye
zahanati akiwa peke yake,”amesema Bugumbi.
“Katika Mafunzo shirikishi haya kwa upande
wangu binafsi naishukuru sana Wizara ya Afya kuanzia leo najua uzazi wa Mpango
ni nini kwa hiyo mimi kama kijana nimeweza kuelewa katika Uzazi wa Mpango na
pia nimeelewa namna ya upatikanaji wa bima hasa tunapoelekea katika Mapango wa
Bima ya Afya kwa Wote na tutakavyonufaika na bima hiyo”amesema kijana
Mletwa.
.
No comments:
Post a Comment