WATU 14 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA MAPANGA DR CONGO - MBUNGE - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Monday, 9 January 2023

demo-image

WATU 14 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA MAPANGA DR CONGO - MBUNGE

image1024x768
Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi.

TAKRIBANI watu 14 wameuawa na wengine 36 hawajulikani walipo kufuatia shambulio katika kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa mbunge wa eneo hilo.

Washambuliaji walikuwa na mapanga walipovamia kijiji hicho siku ya Jumapili huko Djugu katika jimbo la Ituri, alisema Gratien Iracan.

Chanzo kimoja cha ndani kilichozungumza bila kutaka jina lake litajwe kiliiambia BBC kwamba mauaji hayo yanahusishwa na uhasama kati ya makundi ya wanamgambo wanaoendesha shughuli zao katika eneo hilo kufuatia mauaji ya mwalimu wa eneo hilo siku ya Jumamosi.

Msemaji wa jeshi aliiambia BBC kwamba uchunguzi umeanza kuhusu tukio hilo. Mkoa wa Ituri umekuwa ukishuhudia mapigano kati ya makundi ya wanamgambo kuhusu mivutano ya kikabila na umiliki wa migodi ya dhahabu.

-BBC

Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *