KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA KASI UJENZI DARAJA LA PANGANI - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Friday, 14 March 2025

demo-image

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHISHWA KASI UJENZI DARAJA LA PANGANI

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.32_4b5eb098

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.32_5630e918

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.32_f734b1ce

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.33_4de5666c

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.33_9735faa3

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.33_93202a7a

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.34_5b55d801

WhatsApp%20Image%202025-03-14%20at%2017.14.34_e146fb08

MWENYEKITI wa Kamati hiyo Mhe. Seleman Moshi Kakoso amesema kazi iliyofanywa kwenye daraja hilo lenye urefu wa meta 525 ni kubwa hivyo Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), wahakikishe daraja hilo linakamilika kwa wakati ili kukuza fursa za uwekezaji katika ushoroba wa fukwe za mikoa ya Tanga na Pwani.

Hakikisheni kasi ya ujenzi wa daraja iendane na ujenzi wa barabara ili vikamilike na kutoa huduma mara moja", amesema Kakoso.

Kamati hiyo inayoendelea na ukaguzi wa miradi ya kimkakati katika mkoa wa Tanga  imekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani- Bagamoyo Km 256 ambayo ujenzi wake unaendelea.

Naibu Waziri wa  Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya ameihakikishia Kamati hiyo ya Bunge kuwa barabara ya Tanga-Pangani ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 75 itakamilika Juni mwaka huu.

" Tumejipanga kuhakikisha sehemu hii ya kwanza Tanga-Pangani inakamilika ifikapo mwezi Juni wakati daraja likitarajiwa kukamilika Disemba mwaka huu", amebainisha Naibu Waziri Kasekenya.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Mohamed Besta amesema ujenzi huo umegawanywa katika sehemu nne ili kuharakisha ujenzi wake.

Amezitaja sehemu hizo kuwa ni Tanga-Pangani km 50, daraja la Pangani meta 525 na barabara unganishi km 25.6, barabara ya Mkange-Mkwaja-Tungamaa km 95.2 na sehemu ya Mkange-Bagamoyo Makurunge km 73.25 ambayo usanifu wake umekamilika.

Kukamilika kwa barabara hii  kutachochea ukuaji wa uchumi, kupunguza gharama na muda wa safari, kuwezesha kufikika kwa urahisi vivutio vya utalii na kuunganisha kwa njia fupi bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO TANROADS

Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *