TUMIENI BANDARI YA MTWARA KIKAMILIFU PROF. MBARAWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 2 December 2022

TUMIENI BANDARI YA MTWARA KIKAMILIFU PROF. MBARAWA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa bandari ya Mtwara ambayo imefanyiwa maboresho ya kimiundombinu na vifaa alipokagua bandari hiyo leo,(wapili kushoto), ni Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Eng. Juma Kijavara akifuatilia.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Eng. Juma Kijavara (kushoto), alipokagua bandari hiyo leo.

Kaimu Meneja wa bandari Mtwara Bw, Nobert Kalembwe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagua bandari hiyo leo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Eng. Juma Kijavara (kushoto), alipokagua bandari hiyo leo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Eng. Juma Kijavara na Kaimu Meneja wa bandari Mtwara Bw, Nobert Kalembwe wa kwanza kushoto alipokagua bandari hiyo leo.

Kaimu Meneja wa bandari Mtwara Bw, Nobert Kalembwe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagua bandari hiyo leo.

Muonekano wa mtambo wa kisasa wa kupakia na kupakuwa mizigo melini ambao umefungwa katika bandari ya Mtwara.

Kaimu Meneja wa bandari Mtwara Bw, Nobert Kalembwe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagua bandari hiyo leo.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wadau wa usafirishaji na wafanyabiashara wa ukanda wa kusini kutumia kikamilifu bandari ya Mtwara ambayo imefanyiwa maboresho makubwa ya kimiundombinu na vifaa.

Amesema hayo mjini Mtwara mara baada ya kukagua mtambo wa kisasa wa kushusha na kupakia mizigo bandarini hapo (SSG), na kusisitiza kuwa baada ya kuboresha bandari hiyo meli kubwa sasa zinaweza kuitumia na hivyo kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es salaam.

“Baada ya kuboresha bandari hii sasa tunaweza kupokea meli kubwa zenye tani elfu 60, tumepunguza tozo zinazosimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambazo ni gharama za usafirishaji na za kupakia na kupakua mizigo melini”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, amesisitiza kuwa bandari ya Mtwara sasa ina kituo cha kupokelea mafuta hivyo kutoa wito kwa nchi jirani ikiwemo Malawi kutumia bandari hiyo ili kuleta tija kwa kunufaika na punguzo la tozo na huduma za haraka na salama.

Amehimiza viongozi wa TPA kuitangaza kitaifa na kimataifa ili meli nyingi zitumie bandari hiyo na kuchochea uchumi wa mikoa ya kusini na Mtwara kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Eng. Juma Kijavara amesema TPA imejipanga kujenga mtambo wa kisasa wa kupakia makaa ya mawe conveyor belt ili kupunguza athari za kimazingira na kiafya kwa wananchi.

Amesema TPA imeandaa mkakati wa kujitangaza ili wadau wa bandari, wananchi na wafanyabiashara watambue fursa mpya zinazotolewa na kunufaika nazo kwa wakati.

Katika hatua nyingine Waziri huyo wa ujenzi amezungumzia kufurahishwa kwake na kasi ya maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa kiwanja wa ndege wa Mtwara na kusisitiza nia ya Serikali ni kuhakikisha kiwanja hicho kinatoa huduma za kisasa na kimkakati katika ukanda wa kusini.

Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Mtwara (TANROADS), Eng. Dotto John amesema maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mnivata-Masasi km 160 kwa kiwango cha lami yanakwenda vizuri ambapo zaidi ya shilingi bilioni 279, zinatarajiwa kutumika.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI


No comments:

Post a Comment