UJIRANI MWEMA NA TANZANIA MUHIMU KATIKA MAPAMBANO YA EBOLA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 12 October 2022

UJIRANI MWEMA NA TANZANIA MUHIMU KATIKA MAPAMBANO YA EBOLA

 




Na Faustine Gimu, Bugango Uganda/Tanzania 

BAADHI ya raia wa Uganda wamesema  ushirikiano na ujirani mwema Tanzania umekuwa  nguzo muhimu katika kupambana na ugonjwa wa Ebola kwa kuweka mikakati ya pamoja katika kuzingatia kanuni za afya hasa mipakani.

Wakizungumza katika Kijiji cha Bugango upande wa Uganda, baadhi ya raia wa Uganda akiwemo Mulikatete Jesca pamoja na Gaspary Kundii wamesema hatua hiyo ya ujirani mwema imekuwa  ni msingi mkubwa kwa kusaidiana masuala mbalimbali ikiwemo ikiwemo hatua za kuzingatia kupambana na Ebola.

“Sisi na Tanzania tunaujirani mwema hatuna shida yoyote, tunapoenda Tanzania tunahudumiwa, tunanawa na Jick [sanitizer], tunapewa huduma zote za afya bila shida yoyote,“ amesema Mulikatete.

Nao baadhi ya viongozi wa kijiji cha Bugango kwa upande wa Tanzania akiwemo mwenyekiti wa kijiji Meshack Masumbuko pamoja na mtendaji wa kijiji Anthony Jovenary wamesema wamekuwa na mkakati wa kuitisha mikutano ya pamoja kwa pande zote kwa ajli ya kuwekeana taratibu za kuzingatia kanuni za afya hali ambayo imesaidia kanuni za afya kuzingatiwa mipakani.

Kwa upande wake Mganga mkuu mkoa wa Kagera Dkt, Issessanda Kaniki amesema wameweka mbinu ya pamoja  katika utoaji wa huduma na ufuatiliaji wa pamoja tetesi za wahisiwa wa Ebola na ukaguzi wa wasafiri kwa pande zote mbili.

“Tunashirikiana kuweza kutoa taarifa na kutoa huduma iwapo mtu atatokea” amesema Dkt. Kaniki.

No comments:

Post a Comment