Msimamizi wa ujenzi wa chuo hicho, Daudi Mrutu (kushoto) akitoa maelezo ya ujenzi wa chuo hicho kwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye (wa nne kutoka kulia. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Widege Mzalendo, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Dodoma, John Mwanja na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Ikungi, Erick Nyoni.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Dodoma, John Mwanja (wa pili kulia) akitoa maelezowakati wa ukaguzi wa jengo la utawala wa chuo hicho.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Widege Mzalendo (kushoto) , akielekeza jambo wakati wa ukaguzi huo.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye (katikati) akiangalia baadhi ya samani zilizonunuliwa kwa ajili ya chuo hicho.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro wakati wa mkutano wa kupata taarifa ya ujenzi uliofanyika ukumbi wa chakula wa chuo hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Mika Likapakapaaakizungumza katika mkutano huo.. Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Stamili Dendego na kulia ni Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Widege Mzalendo.
Mkutano ukiendelea.
Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ikungi. Kutoka kulia waliosimama mbele ni ni Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Ikungi, Erick Nyoni, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida,Widege Mzalendo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Jerry Muro, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Mika Likapakapa na Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Dodoma, John Mwanja. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Suzana Kidiku na kushoto kwake ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Winfrida Funto.
Na Dotto Mwaibale, Singida
NAIBU Mkurugenzi wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Neema Mwakalyelye ameipongeza
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA)-Kanda ya Kati-Dodoma kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi wa Chuo cha
Ufundi cha VETA Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Mwakalyelye alitoa pongezi hizo juzi wakati akizungumza na viongozi wa
Wilaya ya Ikungi wakiwepo wajumbe wa kamati ya ulizi na usalama wa wilaya
hiyo alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kutembelea chuo hicho na kukagua ujenzi wake uliofanywa na VETA Kanda ya kati kwa kusimamiwa na TAKUKURU.
Aliwapongeza VETA kwa kukamilisha ujenzi huo kwa muda mfupi na kuwa amefarijika
sana na kama wanavyofahamu Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa miradi ya
namna hiyo ya kimkakati na akasisitiza kuwa litakuwa ni jambo la kuvunja moyo na kuhuzunisha pale
ambapo kutakuwa na ufujaji au upotevu wa utekelezaji wa mradi ambao hauonekani moja kwa moja lakini
unaonekana katika viwango vya mradi husika.
“Nifaraja nimekuja na kuona hatua mliyofikia majengo mliyojenga na
miundombinu ipo katika viwango tarajiwa vinavyotakiwa na Serikali na hilo nalo ni
sababu nyingine ya kuwapongeza wale wote mlioufikisha ujenzi huu katika hatua
hii nzuri licha ya mradi kuwa na changamoto kubwa” alisema Mwakalyelye.
Alisema VETA wanakuwa mfano
wa kuigwa kwa sababu miradi ya namna hiyo inaendelea katika sehemu mbalimbali
ya nchi na kama mkurugenzi alivyosema kuwa nia ya Serikali ni kuwa mwaka wa
fedha ujao kila wilaya ambazo ni takribani 62 zitakuwa na miradi yenye sura kama hiyo ikiendelea.
Alisema kutokana na hali
hiyo hatarajii kusikia VETA amekwenda Waziri Mkuu kufungua mradi wa chuo na
kukutana na sintofahamu kwa sababu Ikungi
wanauzoefu wa kutosha wa kuonesha miradi ya namna hiyo inaweza kufanyika na
thamani ya fedha ikaonekana na kupatikana .
“Nimtake Mkurugenzi wa VETA
Kanda ya Kati Dodoma John Mwanja ampelekee ujumbe huu Mkurugenzi Mkuu wa VETA
nchini kuona kwamba miradi kama hii inayofanywa vizuri itumike kama miradi ya
mafunzo ya ndani kwa ajili ya kujengeana uwezo katika maeneo mengine ambayo
miradi ya namna hiyo inapelekwa” alisema Mwakalyelye..
Alisema haitakuwa na maana
kuona mradi wa Ikungi umekamili vema lakini baada ya siku au miezi kadhaa
katika maeneo mengine eti mkuu wa chuo au mkurugenzi wa kanda wa VETA
wamesimamishwa kwa ujenzi uliochini ya kiwango hivyo kwa uzoefu huo walioupata
Ikungi wautumie katika maeneo mengine ili kuepuka hasara inayoweza kutokea
kutokana na watu wasio na ufahamu kamili au kuwa na nia ovu ambapo aliomba
wapewe ushirikiano katika uendelezaji wa wilaya hiyo ambayo inakuwa kwa kasi
kubwa.
Aidha Mwakalyelye aliwataka
viongozi wilayani humo kuhakikisha wanasimamia vizuri ununuzi wa mbembejeo za kilimo
na mapato yote yanayokusanywa yanaingizwa kwenye akaunti za Serikali na si
vinginevyo.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya
Kati John Mwanja akitoa taarifa ya ujenzi wa chuo hicho alisema Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ikungi chenye umiliki wa Hati
namba: 2218- SGD kinajengwa katika
Kijiji cha Muungano,Kata ya Unyahati wilayani
Ikungi katika mkoa
wa Singida kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 50.
Alisema Mradi huo ulianza mnamo
mwezi Machi, 2020 ukisimamiwa na chuo cha VETA Singida na ulipaswa kutekelezwa
kwa muda wa miezi sita hata hivyo, haukuweza kukamilika kwa wakati kutokana na
changamoto kadhaa zilizojitokeza na baadaye mradi kusimama kwa muda wa mwaka
mmoja.
Alisema Mkurugenzi Mkuu wa VETA Februari 28/2022 alihamishia majukumu
ya usimamizi wa Ujenzi wa chuo hicho kutoka Chuo cha VETA Singida kwenda ofisi
ya Mkurugenzi wa VETA Kanda ya kati
ambaye hadi sasa ndiye anaendelea na usimamizi wa ujenzi huo ambao unatekelezwa
kwa mfumo wa “Force Account”.
Akizungumzia utekelezaji wa ujenzi huo alisema unahusisha jumla ya
majengo 17 ambayo ni Jengo moja la utawala, Majengo manne ya karakana, jengo moja la madarasa mawili
makubwa, majengo mawili ya mabweni (Wasichana na Wavulana), Bwalo la chakula na
Jiko, Majengo Matatu ya vyoo (Wasichana Wavulana na
Watumishi), nyumba mbili za watumishi,
jengo la umeme,
Jengo la bohari
na kibanda cha mlinzi. Kwa wastani hatua ya ujenzi hadi sasa
imefikia asilimia 96.
Mwanja alisema mradi wa ujenzi wa chuo hicho unatarajiwa kukamilika
mwishoni katikati ya mwezi Novemba, 2022 na kuwezesha kutoa nafasi ya kufanya
ukamilishaji wa taratibu zingine zenye kuwezesha utoaji wa mafunzo katika chuo.
Alisema chuo
kitakapokamilika, kitaendesha mafunzo ya kozi ndefu na fupi na kkuwa ya muda
mrefu yatachukua muda wa miaka miwili hadi mitatu ambayo yatatolewa katika fani zipatazo sita katika
awamu ya kwanza mara chuo kitakapokamilika ambazo ni Uhazili na Kompyuta
(Secretarial and Computer Application),Ushonaji (Design Sewing and Cloth
Technology), Uashi (Masonry and Bricklaying),Umeme wa Majumbani (Electrical
Installation),Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics) na Uchomeleaji Vyuma
(Welding and Metal Fabrication).
Alisema chuo kitakuwa na
uwezo wa kudahili
wanafunzi 240 wa
kozi ndefu na
uwezo wa kuchukua wanafunzi 144 wa bweni (wasichana 64 na wavulana 80).
Alisema pia, kutakuwa na mafunzo ya muda mfupi (Short Courses) yatakayochukua muda wa mwezi mmoja hadi miezi sita kwa wastani mafunzo hayo yanakadiriwa kudahili wanafunzi wapatao 250 hadi 900 kwa mwaka kutegemeana na mahitaji ya jamii na shughuli za kiuchumi za eneo hilo.
No comments:
Post a Comment