POSTA SINGIDA YAFANYA MABORESHO MAKUBWA YA KITEKNOLOJIA KWENYE UTOAJI HUDUMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 10 October 2022

POSTA SINGIDA YAFANYA MABORESHO MAKUBWA YA KITEKNOLOJIA KWENYE UTOAJI HUDUMA

Wafanyakazi wa shirika la Posta Mkoa wa Singida wakishiriki zoezi la kufanya usafi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyofanyika jana mkoani hapa. Wa pili kulia ni  Meneja wa Posta mkoani hapa, Michael Mwanachuo.

Picha ya pamoja.

Picha ya pamoja.

Ufanyaji usafi ukiendelea. Kushoto ni  Meneja wa Posta mkoani hapa, Michael Mwanachuo.

Ufanyaji usafi ukiendelea.

Wafanyakazi hao wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa zoezi hilo la kufanya usafi.

 Meneja wa Posta mkoani hapa, Michael Mwanachuo (kushoto) akiwalisha keki ikiwa ni moja la tukio katika kusherehekea wiki hiyo ya huduma kwa wateja.

Keki ikiliwa.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Godwin Myovela, Singida

KAULI Mbiu inayovuma kwa kasi ya Shirika la Posta nchini (TPC) isemayo ‘Posta Twenzetu Kidijitali-Haijawahi Tokea! imezidi kujidhihirisha kupitia ofisi za shirika hilo mkoani hapa, ambapo kupitia wiki ya huduma kwa wateja, mamia ya wananchi wameonyeshwa kufurahishwa na maboresho ya kihuduma yanayoendelea kutolewa kwa sasa.

 Akizungumza muda mfupi baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira na kutoa faraja kwa wagonjwa ndani ya hospitali ya mkoa wa Singida-kama azma yake kwenye ushiriki wa majukumu ya kijamii, Meneja wa Posta mkoani hapa, Michael Mwanachuo, pamoja na mambo mengine alisema mwaka huu shirika hilo limekuja kivingine.

Alisema wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, inayokwenda sambamba na shamrashamra za shirika hilo kuelekea kilele cha siku ya Posta Duniani ambayo huadhimishwa ifikapo Oktoba 9 kila mwaka shirika kwa kuzingatia mifumo ya kasi ya TEHAMA linaendelea kusafirisha barua kwa njia ya haraka (EMS) ndani na nje ya nchi na usafirishaji mizigo mikubwa.

Pia kwa kutumia TEHAMA ya Posta Kiganjani ambayo humwezesha mteja yeyote kupata huduma za posta popote, Mwanachuo alisema mpaka sasa fursa mbalimbali kwa matokeo bora na ya uhakika zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia kasi na ufanisi, ikilinganishwa na siku za nyuma.

“Posta kwa sasa tupo kidijitali zaidi nitoe wito kwa umma kuzidi kutembelea ofisi za shirika letu na kutuunga mkono kwa kujipatia huduma zetu mbalimbali za kidijitali zilizoboreshwa.” Alisema Mwanachuo.

Shirika hilo kwa sasa pamoja na mambo mengine linatoa huduma za kidijitali za Uwakala wa Fedha, Masanduku ya Barua, Duka Mtandao, Intaneti Café, na mfumo madhubuti wa kufuatilia barua au kifurushi kilichotumwa kupitia mtandao kujua kimefikia wapi au kimepokelewa na nani.

Huduma nyingine ni pamoja ‘Posta Cash’, Uwakala wa Bima, Huduma za uuzaji wa hisa za makampuni mbalimbali na huduma za Bodi ya Mikopo na Baraza la Mitihani sanjari na huduma kwa wananchi wanaohitaji vyeti vya kuzaliwa ambapo kazi ya kujaza fomu na nyaraka zote ni sehemu ya majukumu ya shirika hilo ambapo mwananchi akikamilisha taratibu zote anakwenda kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa hatua ya mwisho ya kuchukua cheti.

Shamrashamra hizo zilipambwa na shughuli mbalimbali kwa shirika hilo mkoani hapa kufanya usafi wa mazingira, utoaji wa huduma za kidijitali sanjari na kujumuika kukata na kula keki na wateja wake ‘wakiwemo wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Big Stars’ kama sehemu ya kurudisha shukrani.

No comments:

Post a Comment