RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS WA KENYA DK. WILLIAM RUTO, KENYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 13 September 2022

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS WA KENYA DK. WILLIAM RUTO, KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Kenya katika Sherehe za Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto zilizofanyika kwenye uwanja wa Kasarani, Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.

 


Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto akiwa katika hafla ya uapisho wake Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Rigathi Gachagua mara baada ya Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.

Matukio katika hafla ya uapisho wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto akiwa katika hafla ya uapisho wake Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na baadhi ya Marais wa nchi mbalimbali katika Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Dkt. William Samoei Ruto kabla ya uapisho Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 13 Septemba, 2022.

No comments:

Post a Comment