KIFO cha Malkia Elizabeth II kimeangazia tamaduni za maombolezo na zisizo za kawaida nchini Uingereza, ambazo nyingi zimesambaa kote duniani. Sawa na mambo mengi yanayohusisha Familia ya Ufalme wa Uingereza, kipindi chama maombolezo cha kifo cha Malkia hufanyika kwa tamaduni na mikataba.
Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II tarehe 8 Septemba, kipindi cha maombolezo ya kifalme kilitangazwa, ambacho kitaisha siku saba baada ya mazishi. Hii ni sehemu ya historia kuhusu baadhi ya tamaduni ambazo zinatumiwa katika kifo cha Malkia ambaye amehudumu zaidi katika ufalme wa Uingereza, ambazo zimekuwa maarufuu katika maeneo mbali mbali duniani.
Mojawapo ya njia rasmi ya kuonyesha kipindi cha maombolezo ni kushusha bendera na kuipeperusha nusu mlingoti katika majengo ya serikali na yale yanayohusika na Familia ya Ufalme. Huku neno nusu mlingoti hutumika, ukweli ni kwamba bendera hupeperushwa theruthi mbili ya mlingoti.
Ni utamaduni ambao unaaminiwa kuanza kutekelezwa katika karne ya 17 – kwa kushusha bendera, mtu hutoa fursa ya kwa ajili ya ishara "isiyoonekana ya kifo cha bendera" juu ya bendera ya kawaida.
Utamaduni huu ulianza kama heshima kwa kifo cha nahodha au afisa wa ngazi ya juu wa meli. Wafanyakazi wengine wa meli walikuwa wakiomboleza kifo kwa kushusha bendera ya meli. La kushangaza ni kwamba licha ya kwamba sheria hii haitekelezwi kwa kiwango cha Ufalme, bendera iliyopeperushwa ni ishara ya uwepo wa uhuru.
Huwa haipeperushwi nusu mlingoti kwasababu ufalme huendelea – wakati kifo cha Malkia Elizabeth II kilipotokea, Mwanamfalme Charles, mwanaye mkubwa zaidi moja kwa moja alikuwa Mfalme Charles III.
Bendera nyingine nchini Uingereza zitapepea nusu mlingoti hadi saa mbili asubuhi siku moja baada ya mazishi. Katika mazishi ya kitaifa ya Malkia, jambo la kipekee likiwa ni siku ya Baraza linalomtangaza mrithi wa Ufalme tarehe 10 Septemba wakati Mfalme alitangazwa rasmi.
Katika siku hiyo bendera zilipandishwa na kufikia juu ya mlingoti kwa saa kadhaa kuadhimisha tukio hilo kabla ya kurejeshwa tena nusu mlingoti. Utamaduni mwingine unaohusiana na maombolezo ya wafalme ni heshima ya kufyatuliwa kwa mizinga.
Kulingana na wanahistoria wa jeshi la Uingereza, utamaduni huu ulianza katika karne ya 15 wakati meli za kivita zilipokuwa zikitembelea bandari za kigeni zilikuwa zikifyatua mizinga baharini ili kutoa ishara kwamba walikuwa wanakaribia kwa lengo la amani kwasababu silaha zao zilikuwa tupu.
Kufikia mwaka 1730 jeshi la wanamaji la Uingereza, tayari lilikuwa linatumia heshima za mizinga uadhimisha baadhi ya matukio, ingawa haikuwa lazima kwa ajili ya Familia ya Ufalme na wakuu wengine wa kitaifa, hadi ilipofika mwaka 1808. Kulikuwa na sheria tata zinazoelezea idadi ya mizinga, ambayo inategemea ni wapi ilikuwa inafyatuliwa, na kwa tukio gani.
Katika mwaka 1827 agizo la Bodi ya usalama wa silaha iliagiza kuwa mizinga 41 ni sahihi ni sahihi kwa heshima ya Ufalme wakati inapofyatuliwa kutoka eneo la bustani za ufalme-Royal Parks, mjini London au kutoka kwenye Mnara wa London - Tower of London.
Lakini katika baadhi ya matukio katika baadhi ya maeneo idadi ya mizinga inayofyatuliwa huongezwa na kufikia 62. Mizinga ya heshima imekuwa ikifyatuliwa katika maombolezo ya Malkia Elizabeth II na kuadhimisha kutawazwa kwa Mfalme Charles III.
Tarehe 9 Septemba, siku moja baada ya kifo cha Malkia, mizinga ilifyatuliwa katika eneo la Hyde Park mjini London, huku mzinga mmoja ukifyatuliwa kwa ajili ya kila mwaka wa miaka 96 ya maisha yake aliyoishi.
Makanisa ya Kanisa la England , makanisa madogo na Makanisa makuu yalipiga kengele zao siku alipofariki Malkia Elizabeth II.
Kifo cha mtawala wa ufalme ni moja ya matukio ya nadra ambapo sauti za kengele – ambapo hupigwa kwa ufundi wa kipekee wa kupigwa ambazo hutoa mwangwi unaotoka katika pande zote za kengele. Lakini baadaye kengele hupigwa kikamilifu kuadhimisha tukio la kusimikwa kwa mfalme.
Katika England, utamaduni huu unadhaniwa kuanza katika karne ya 7 kama ilivyotajwa katika maandiko ya mtawa Venerable Bede kuhusu kifo cha Hilda of Whitby ambaye aliishi katika kipindi hicho. Mojawapo ya utamaduni wa kipekee wa Familia ya Ufalme ni kupiga kengele za Sebastopol Bell Katika Kari ya Windsor.
Wakati wa vita vya Crimean katika mwaka 1856, kengele zilishikiliwa na Warusi na kuchukuliwa kutoka katika kanisa la Manabii kumi na wawili katika Sebastopol na kupelekwa katika kasri ya ufalme.
Siku moja baada ya kifo cha Malkia ilipigwa mara moja kwa kila mwaka alioishi, utamaduni unaofanyika kwa ajili ya maafisa wa ngazi ya juu pekee wa Familia ya Ufalme. Kengele hiyo ilipigwa kuadhimisha kifo cha mama yake Malkia katika mwaka 2002.
Taarifa fupi – katika karatasi iliyotundikwa kwenye fremu ndogo ya ubao – hutumiwa kuufahamisha umma kuhusu matukio muhimu ya ufalme kama vile kuzaliwa au vifo katika Buckingham Palace. Kwa uzazi, fremu huwekwa katika rangi ya dhahabu na huwekwa katika uwanja wa mbele ya kasri, ndani ya uzio, kwa vifo fremu huwa kwa kawaida inawekwa nje ya uzio.
Vifo vya George VI, katika mwaka 1952, na George V, katika mwaka 1936, pia vilitangazwa kwa njia hii.


No comments:
Post a Comment