WAZIRI DKT. GWAJIMA AIPONGEZA JAMES FAOUNDATION - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 28 May 2022

WAZIRI DKT. GWAJIMA AIPONGEZA JAMES FAOUNDATION


Na MJJWM, Dar

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima kuelekea Siku ya Mtoto amelipongeza Shirika la James Foundation kwa jitihada zake na ubunifu wanaoufanya katika mapambano dhidi ya Ukatili nchini.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo Mei 27, 2022 wakati wa Uzinduzi wa Stika za kampeni ya namba 116 kwa ajili ya kufichua viashiria na Vitendo vya Ukatili ikiwani ni kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 16, Juni.

"Nawapongeza sana James Foundation kuja na mkakati huu kuelekea Juni 16 Siku ya Mtoto wa Afrika tunapoelekea kwenye kilele cha Siku hiyo, tumesema lazima kila mdau aje na mawazo mbadala kama wenzetu James Foundation" alisema Dkt. Gwajima

Pia Dkt. Gwajima alisema watafanya kampeni ya kujitolea ili kufanya jamii kuwa salama huku kila mmoja  akitakiwa kupaza sauti na kusema ukatili sasa basi kwani hatutaweza kushinda vita hii kwa mali na fedha bali kwa nguvu ya umoja kwenye kuelimisha kubadili fikra.

Aliongeza kuwa kila mwanajamii anatakiwa kushiriki kwani matukio ya ukatili kwa watoto yanatokea Majumbani kwa  asilimia 60 hivyo bila kupambana kwa kushikamana kwa hamii ni vigumu kushinda vita hiyo.

"Serikali inafurahi kuona kwamba wanajamii wenyewe, Taasisi mbalimbali, Sekta Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, hususan Shirika la James Foundation zinaungana katika azma ya kutetea haki na wajibu wetu wa kulinda haki hizo, na kupinga vitendo vyote vya kikatili na unyanyasaji wa kijinsia." alisema Dkt. Gwajima.

Awali akisoma Risala  Athanas Alphonce kutoka James Foundation, alisema Taasisi yao imejipambanua katika kuhakikisha wanatatua tatizo la watoto wa mitaani ambao wengi wao wanapita kwenye Janga la Ukatili.

"Tunafanya hayo kwa kushirikiana na Wizara yako Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Jeshi la Polisi, na Wadau Mbalimbali wa Maendeleo. alisema Athanas

Naye Mwakilishi wa Jeshi la Polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam dawati la Jinsia Mkaguzi Msaidizi  M. K  Makora
 alisema tatizo la ukatili ni kubwa tofauti na wengi wanavyokutazama hivyo Suluhu pekee ni kwa wadau wote kushikamana wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi sambamba na wananchi wenyewe kutoa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment