WATUMISHI WA SEKTA YA UCHUKUZI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTOA FEDHA KWA AJILI YA MRADI WA RELI YA KISASA YA SGR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 29 May 2022

WATUMISHI WA SEKTA YA UCHUKUZI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTOA FEDHA KWA AJILI YA MRADI WA RELI YA KISASA YA SGR

 

Meneja Mradi Msaidizi Sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro (KM 300) , Mhandisi Thadei Paul, akieleza kwa watumishi wa Sekta ya Uchukuzi namna abiria watakavyoshuka katika treni ya Kisasa ya SGR katika stesheni kuu ya Tanzanite jijini Dar es Salaam, wakati walipotembelea mradi huo sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.

Meneja Mradi Msaidizi Sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro (KM 300) , Mhandisi Thadei Paul, akieleza kwa watumishi wa Sekta ya Uchukuzi namna treni ya Kisasa ya SGR zitakavyofanyiwa ukarabati katika karakana iliyopo Kwala, Mkoani Pwani, wakati walipotembelea mradi huo, mwishoni mwa wiki, Mkoani Pwani.

Mhandisi wa Reli wa Kisasa ya SGR, Sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro (KM 300), Moses Matoholo akieleza kwa watumishi wa Sekta ya Uchukuzi namna abiria watakavyotumia tiketi zao katika stesheni ya Morogoro wakati walipotembelea mradi huo, mwishoni mwa wiki, Mkoani Morogoro.

Meneja Mradi Msaidizi Sehemu ya Morogoro hadi Makutupora (KM 422), Mhandisi Oliva Kilyenyi, akieleza  kwa watumishi wa Sekta ya Uchukuzi namna abiria watakavyoingia na kutoka katika stesheni ya Kilosa, wakati walipotembelea mradi huo, mwishoni mwa wiki, Mkoani Morogoro.

Meneja Mradi Msaidizi Sehemu ya Morogoro hadi Makutupora (KM 422), Mhandisi Oliva Kilyenyi (Aliyevaa Kofia ngumu nyeupe) katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekta ya Uchukuzi wakati walipotembelea mradi huo, mwishoni mwa wiki, Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro.

Meneja Mradi Msaidizi Sehemu ya Morogoro hadi Makutupora (KM 422), Mhandisi Oliva Kilyenyi, akieleza kwa watumishi wa Sekta ya Uchukuzi kuhusu namna mahandaki ya reli ya Kisasa ya SGR jijini Kilosa yalivyojengwa, wakati watumishi hao walipotembelea mradi huo, mwishoni mwa wiki, Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro.

Mkadiriaji Majenzi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Ignas Lyimo akieleza kwa watumishi wa Sekta ya Uchukuzi kuhusu namna kokoto zinavyowekwa kwenye reli ya Kisasa ya SGR, wakati watumishi hao walipotembelea mradi huo sehemu ya Morogoro hadi Makutupora (KM 422), mwishoni mwa wiki, Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment