Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Kibaha Mjini Elina Mgonja akizungumza wakati wa kongamano la kibiashara 2021. |
Na Dunstan Mhilu
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Kibaha Mjini Elina Mgonja amewataka watanzania kuwapuuza wote wanaosema Rais Samia Suluhu Hassan hajafanya chochote katika uendelezaji wa miradi iliyoachwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano hayati Dk John Magufuli.
Alisema hayo jana wakati akizungumza na HabariLEO katika ofisi za UWT Kibaha mjini na kueleza kuwa jambo hilo halivumiliki na kwa mtu mwenye utashi hawezi kulubuniwa na maneno ya wachache ambao kwa chuki zao hawaoni kuwa Rais Samia kafanya chochote jambo ambalo si la kweli.
"Ndugu zangu watanzania tuwapuuze wote ambao wanamdhihaki Mama yetu Rais Samia Suluhu kuwa hakufanya chochote, huo ni uongo na uzushi na tabia ya aina hii haivumiliki, Rais alitekeleza miradi ya maendeleo akiwa ni msaidizi wa mtangulizi wake kama hiyo haitoshi aliposhika hatamu tu aliutangazia Umma wa watanzania kuwa ,kazi iendelee, alisema Elina.
Aliongeza kuwa Rais Samia anaupiga mwingi kwakuendeleza miradi ya awali na kuibua miradi mipya hivyo hastahili dhihaka na fedhuli bali anahitaji heshima na adabu kama kiongozi Mkuu wa nchi"alisema Elina.
Mwenyekiti huyo alisema kama Chama lazima kikisemee Chama na serikali kwakuelimisha umma mazuri yanayofanywa na Rais wao kwani kukaa kimya ni kufanya uongo kuwa kweli kitu ambacho si sahihi.
Elina amewasihi watanzania kujitokeza Agosti 23 mwaka huu kuhesabiwa kwa manufaa yao na nchi na kuachana na hila na propaganda za kisiasa zisizo wanufaisha kwakuwa zinafanywa na vikundi vichache vya watu kwa manufaa Yao.
Naye Katibu wa UWT Kibaha Mjini Mariam Mgasha amempongeza Rais Samia kwakutatua changamoto mbalimbali nchini na kuwa mbunifu katika kuwaletea maendeleo wananchi.
“Kwakipindi Cha mwaka mmoja Rais Samia ameupiga mwingi hususani kuwapigania Wanawake kwakuongeza kima Cha chini Cha mshahara kwakuwa Wanawake hunufaika mara mbili, Kuna wanaonufaika kupitia waume zao, ndugu zao na watoto wao lakini pia wapo wanaonufaika kupitia wao wenyewe kwakuwa nao ni wafanyakazi.
Aidha amempongeza Rais Samia na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Nape Nnauye kwakusimamia vizuri zoezi la uandaji wa Anwani za makazi.
"Kukamilika kwa mfumo huo hivi karibuni itarahisisha mawasiliano ya kibiashara na Utawala nchini sanjari na masuala ya utalii nchini hivyo naipa Tano serikali yetu shime tuiunge mkono kwakufanya kazi kwa bidii, viva Tanzania, Viva UWT na viva CCM" alisema Mariam.
No comments:
Post a Comment