Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani Christopher Myava akizungumza na vyombo vya Habari picha na Maktaba. |
Na Dunstan Mhilu
MKUU wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKURU) Mkoa wa Pwani Christopher Myava ametoa onyo watu wanaijihusisha na utapeli wa ardhi mkoani humo.
Myava alitoa onyo hilo alipokuwa alipokuwa akizungumza na HabariLeo katika Ofisi ya Takukuru Mkoa wa Pwani wilayani Kibaha.
Alisema hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi kudhulumiwa ardhi yao na matapeli huziuza kwa wawekezaji wa ndani na wakigeni waliodhamiria kuwekeza katika mkoa huo ambao ambao upo kimkakati kwa ajili ya viwanda.
"Takukuru Pwani tumejikita zaidi katika kuzuia 'kudhibiti na kupambana vitendo vya Rushwa, hata kama vikitokea visiwe na madhara makubwa, hivyo tunasisitiza kuwa tupo kazini kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya Rushwa haswa rushwa ya ardhi ktika mkoa huu hatakuwa salama," alisema Myava.
Myava alilisisitiza kuwa matapeli wa ardhi mkoani humo si kwamba wanawaumiza tu wawekezaji wa ardhi bali hulichafua Taifa, wakati serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
Akizungumza ubadhirifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo itokanayo na fedha za COVID-19 Myava alisema wanaendelea na ufuatiliaji na uchunguzi wa karibu ili hatua za kisheria zichukuliwe ikiwemo kufunguliwa mashtaka.
"Tulikuwa tukifuatilia miradi ya maendeleo kwa muda mrefu na wakati wa mbio za mwenge zilizoanza Mei, 1,2022 hadi Mei 10 2022 Mkoani Pwani miradi 111 ilipitiwa na mbio za mwenge na michache kubainika kuwa chini ya viwango hivyo basi Takukuru Pwani inaendelea na uchunguzi na hivi karibuni itatoa taarifa hiyo kwa umma kupitia vyombo vya habari" alisema Myava.
Hata hivyo akihitimisha mazungumzo yake na HabariLeo Myava alisema watanzania wana uelewa mkubwa wa masuala ya Rushwa na ndiyo hufanya kazi ya kuzuia na kupambana na Rushwa kuwa rahisi na hiyo imetokanaa na Taasisi hiyo kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuripoti vitendo na viashiria vya Rushwa nchini.
Kwa mujibu wa Myava alisema Tanzania katika rekodi za kimataifa katika kuzuia na kupambana na Rushwa ipo mstari wa mbele na inaridhisha.
No comments:
Post a Comment