UVAMIZI WA UKRAINE: URUSI YAONYA KUWA ITASHAMBULIA MAENEO MAALUM MJINI KYIV - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 1 March 2022

UVAMIZI WA UKRAINE: URUSI YAONYA KUWA ITASHAMBULIA MAENEO MAALUM MJINI KYIV


WIZARA ya ulinzi ya Urusi imetoa onyo kwa wakazi wa Kyiv kwamba inajiandaa kushambulia maeneo maalum katika mji mkuu wa Ukraine.

Katika taarifa iliyotolewa leo mchana, maafisa wa Urusi walisema vikosi vyao vinajiandaa kufanya "mashambulizi ya uhakika na ya hali ya juu" dhidi ya "vituo vya kiteknolojia vya Huduma ya Usalama ya Ukraine na kituo kikuu cha 72 cha PsyOps huko Kyiv".

"Tunawahimiza raia wa Ukraine ambao wanatumiwa na watu wa kitaifa kutekeleza uchochezi dhidi ya Urusi, pamoja na wakaazi wa Kyiv wanaoishi karibu na vituo vya hivyo kuondoka nyumbani kwao," iliongeza taarifa hiyo.

Maafisa walidai mashambuli hilo linafanywa ili "kuzuia mashambulizi ya mawasiliano dhidi ya Urusi".

Huku hayo yakijiri Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov ameonya kuhusu uwezekano wa Urusi kufanya "shambulio la kisaikolojia".

Bw. Reznikov alidai kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa Urusi ikwanza inapanga kuvuruga mawasiliano.

"Baada ya hapo, kutakuwa na usambazaji mkubwa wa taarifa ghushi kuhusu uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Ukraine," aliandika.

Nini kipya kutoka Ukraine?

Huku dunia ikishuhudia siku ya sita ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, fahamu yaliyojitokeza hivi karibuni zaidi:

Katika Kharkiv - mji wa pili wa Ukraine - takriban watu 10 wameuawa na 20 kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa wakati kombora la Urusi lilipopiga makao makuu ya serikali ya mkoa'

Rais wa Ukraine anakiita kitendo hicho "ugaidi dhidi ya serikali" na anaishutumu Urusi kwa uhalifu wa kivita kwasababu hata makazi na raia pia wanashambuliwa, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa watoto 16.

Katika hotuba yake kwa kikao maalum cha bunge la Umoja wa Ulaya, anaomba uwanachama wa muungano huo, akisema itakuwa na nguvu zaidi na Ukraine ndani yake.

Katika mji wa kaskazini-mashariki wa Okhtyrka, hadi wanajeshi 70 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika katika shambulio lililotekelezwa na Urusi.

Wakati huo huo, msafara mkubwa wa magari ya kivita ya Urusi yanasonga mbele kuelekea mji mkuu wa Ukraine Kyiv'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameonekana kutoa uhalali mpya wa uvamizi wa Urusi - akiuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa ni kuzuia Ukraine kupata silaha za nyuklia'

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anaishutumu Urusi kwa mashambulizi ya "kinyama na ya kiholela" na inasema iko tayari kuzidisha vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi kwa muda wote itakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment