MKUU WA WILAYA KIGOMA APONGEZA JUHUDI ZA KULIOMBEA TAIFA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 1 March 2022

MKUU WA WILAYA KIGOMA APONGEZA JUHUDI ZA KULIOMBEA TAIFA

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ujiji, Ester Alexander Mahawe akizungumza wakati wa Ibada ya HIJA hivi karibuni katika viwanja vya Lake Tanganyika.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi akiombea Taifa wakati wa Ibada ya Hija hivi karibuni.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo BABA Halisi akiombea Taifa wakati wa Ibada ya Hija hivi karibuni.

Na Dunstan Mhilu, Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Kigoma Ujiji, Ester Alexander Mahawe amemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba kuendelea kuliombea Taifa. 

 

Hayo yalielezwa jumapili hii wakati wa sherehe za Hija ya Chanzo cha Baraka kwa watu wote, ambapo ibada hiyo ambayo huambatana sherehe kubwa iliyofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika Wilayani humo. 

 

Aliyasema hayo mara baada ya kupokea ujumbe mfupi wa utambulisho wa Kanisa hilo ambalo mapokeo yake na mafundisho ni upendo usiobagua, amani na  ibada ni uzalishaji. 

 

Mkuu huyo wa Wilaya alimshukuru Baba Halisi kwa kuongoza ibada ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, wasaidizi wake na Taifa kwa ujumla.''Nikushukuru sana Baba Halisi kwa maombi ya kumuombea Rais, sisi wasaidizi na Taifa kwani bila dua na maombi hatuwezi kujilinda kwa nguvu zetu wenyewe angalieni kinachoendelea Ukraine na Urusi ni kwasababu amani imetoweka," alisema.

 

Aidha ameushukuru msafara wa maelfu wa mahujaji ambao ni makuhani wa Kanisa hilo kutoka Ndani ya nchi na Mataifa mbalimbali ya Afrika na nchi za Ulaya ikiwemo Jimbo la Boston ambako kuna makuhani wakanisa hilo na hivyo kuingizia Mji wa Kigoma ujiji fedha kupitia vyombo vya usafiri, hoteli, migahawa, maduka, nyumba za kulala wageni na masoko yaliyopo  Manispaa ya Kigoma Ujiji haswa soko la Kibirizi.

 

“Nikushukuru sana Baba Halisi kwakutuletea msafara mkubwa wilayani kwetu ujio wenu umeongeza pato la Mkoa na kaya kwa ujumla kwani wana ujiji wameuza kwelikweli na nikili sijawahi ona msafara mkubwa kama huu hapa Ujiji tokea niwe Mkuu wa Wlaya hivyo jisikieni mpo sehemi salama," alisema.

 

Kwa upande wake kiongozi huyo wa dini alisema ni wajibu wa Kanisa kumuombea Rais, wasaidizi wake na Taifa na kwakuwa DC huyo ameomba basi wataongeza zaidi maombi ili Tanzania na Dunia pawe mahala salama pakuishi

 

Kwakuwa umetuomba tuendelea kuomba tutaendelea zaidi maana ukiwa na shilingi moja hukatai shilingi nyingine," alisema.

 

Vilevile akizungumzia upendo usiobagua kiongozi huyo alisema haijawahi kutokea kwa kizazi cha Ishimail na Isaka kukaa pamoja lakini leo tupo na shehe, maustadhi na maustadhat hili sijambo dogo kwanini tusimshukuru Chanzo Halisi muumba wa vyote pokeeni baraka maana mmefika mlima wasauti, madeni, ukimwi na kama umekuja na ukimwi umetoweka.

 

Kwa upande wake Shehe wa Mkoa wa Kigoma Shehe Alhaj Hassan Kiburwa alisema hakuja peke yake amekuja na mashehe wake wote waswahili wanasema wakati ni ukuta kwahiyo tutumie wakati, huko nyuma hatukuwatambua vizuri lakini sasa tunawaelewa mkifika kigoma inafunguka na mkoa wetu unawapeni kazi yetu ni kuwatoa mashaka tunakupenda umetujengea shule buzebazeba, uhuru, hospitali yetu nguruka kwa michango yetu ingekuwa ngumu kufankisha kwa wakati.

 

Katekista Lazaro Pascal wa Parokia ya Kigoma Ujiji, aliwataka watu wakigoma kusikiliza sauti ya Mungu Kigoma imechelewa kwakukosa mshikamano na historia nzuri ya Kigoma na kumuomba Baba Halisi

 

Wafanyabiashara wa Ujiji wakizungumza na mwandishi wa habari hizi walikuwa na maoni mbalimbali kuhusu tukio hilo la kihistoria.

 

Naitwa Lazaro Nkamba ni mmiliki wa nyumba ya kulala wageni iitwayo Spice kwa kweli ujio wa hawa ndugu umeniingizia mapato na nyumba vyote vimejaa watu wanakuja wanakosa vyumba na wote ni wageni hadi nawaonea huruma," alisema Mkamba.

 

Huko soko kuu la vyakula na samaki la Kibirizi Fatuma Ally anasema kwa hakika hija hiyo imemfanya auze mauzo mengi ya dagaa na migebuka samaki maarufu wavuliwao katika mwambao na mwalo wa Ziwa Tanganyika.

 

Hata hivyo wauza vitenge ambavyo hupatikana kwa wingi kutoka Congo na Burundi na hivyo mahujaji hao kupata fursa ya kuvifungasha kwa wingi kwa kuwa walipata fursa ya kufanya hivyo huku waendesha bajaji na pikipiki wakifurahia ujio huo kwa kupata wateja wengi kutoka kwa mahujaji hao.

 

Kanisa hilo hufanya hija Mkoani Kigoma kila mwaaka hususani mwezi Februari na Machi kama sehemu ya kuukaribisha mwaka wa Kanisa hilo.

 

 


No comments:

Post a Comment