RAIS SAMIA ALIVURUGA TENA BARAZA LA MAWAZIRI, WATANO CHALI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 8 January 2022

RAIS SAMIA ALIVURUGA TENA BARAZA LA MAWAZIRI, WATANO CHALI...!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri, huku akiwaondoa wengine na kuteuwa wapya na kuhamisha baadhi yao.

Katika mabadiliko hayo mawaziri kadhaa wamejikuta wakiondoka katika nafasi zao akiwemo 

Prof. Palamagamba Kabudi, William Lukuvi, Prof. Kitila Mkumbo, Geoffrey Mwambe na Naibu waziri Mwita Waitara.

Akitangaza mabadiliko hayo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu pia.

Rais Samia ''ameunganisha wizara tatu, iliyokuwa wizara ya uwekezaji iliyokuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na pia ameunganisha wizara ya biashara moja ambayo itaitwa uwekezaji, viwanda na biashara'', amesema Balozi Hussein Kattanga.

Aidha kama alivyoahidi Rais Samia ameunda Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia,wanawake na Makundi maalum ikiwa ni kuboresha zaidi utendaji na ufanisi katika Serikali yake. 

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia amemrejesha Nape Nnauye nafasi ya uwaziri ambaye aliondolewa na kuwapandisha manaibu waziri Hamad Masauni, Angelina Mabula na Hussein Bashe kuwa mawaziri kamili.

Wizara ya Habari na teknolojia ya habari sasa itaongozwa na Waziri Nape Moses Nnauye, Wizara mpya ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, itaaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima, Wizara ya Afya itaongozwa na Waziri Ole Mollel, huku Dk. Pindi Chana atakuwa waziri Katika Ofisi ya Waziri Mkuu kushugulikia masuala ya sera Bunge na uratibau.

Dk. Angelina Mabula ataongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiongozwa na Jenista Mhagama, Mohamed Mchengerwa sasa anakuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo huku Waziri Inocent Bashungwa anakuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kwa mabadiliko zaidi ya baraza hilo soma hapa chini:-

                                             










No comments:

Post a Comment