Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu |
WAZIRI wa Afya nchini Tanzania, Ummy
Mwalimu amesema mgonjwa wa kwanza nchini wa virusi vya corona, Isabela
Mwampamba (46) ameshapona ugonjwa huo na mpaka sasa wasafiri 245 wametengwa
kwenye vituo vilivyoandaliwa baada ya kuingia nchini wakitoka nchi zilizoathirika
zaidi na virusi hivyo
Wagonjwa
11 wakiwa wamepatikana Tanzania bara na huku kisiwani Zanzibar kukiwa na
wagonjwa wawili.
Ameongeza
kuwa hakuna maambukizi yaliyopatikana
ndani ya nchi mpaka sasa.
Kesi
mpya ni ya mgonjwa wa Coronavirus aliyepatikana Kagera alikua dereva wa malori
makubwa, ambaye aliingia nchini kupitia mpaka wa kabanga akiwa anaendesha
magari kati ya DRC, Burundi na Tanzania.
Wagonjwa
wote 13 kasoro mmoja wao walisafiri nje ya nchi katika siku 14 zilizopita kabla
ya kuthibitika kuwa na virusi hivyo, na mgonjwa ambaye hakusafiri nje ya nchi
alikutana na muathirika anayetoka nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment