JE, NI GARI GANI ZINATAKIWA KUBEBA KISANDUKU CHA HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID KIT BOX)? - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 26 March 2020

JE, NI GARI GANI ZINATAKIWA KUBEBA KISANDUKU CHA HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID KIT BOX)?

FIRST AID KIT BOX

JE, NI GARI GANI ZINATAKIWA KUBEBA KISANDUKU CHA HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID KIT BOX)?

JIBU
Ni gari za abiria (PSV) na gari za kubeba mizigo ya kemikali tu, kwa mujibuwa sheria ya usafirishaji wa kemikali ya mwaka 2002. Gari nyingine zozote hazilazimiki kuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza ya wagonjwa.

Hoja zenye Sababu(reasoned arguments)
1. Hakuna popote katika sheria ya Usalama Barabarani (ROAD TRAFFIC ACT, cap.168) Tanzania wala kanuni zake panazungumzia au kutaka gari ziwe na kisanduku cha huduma ya kwanza ya wagonjwa.

2. Ni kanuni ya 5(1)(j)(ii) ya Kanuni za LATRA (zamani SUMATRA) zinazohusu Viwango vya kitaalamu na kiufundi vya magari ya Abiria yaani, SUMATRA (Technical Safety and Quality of Service Standards) Passenger Vehicles Rules, GN.14/2008, ambayo ndiyo inayotaka kila gari la abiria kuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza (first aid kit). Hata hivyo, kanuni hizi hazitaji nini kiwemo kwenye hicho kisanduku. Jambo ambalo ni upungufu kwa kanuni hizi. Kanuni tajwa hapo juu zinahusu magari ya abiria pekee.

Aidha, Kanuni ya 23(1)(e) ya Kanuni za Usafirishaji abiria kwa njia ya mabasi ya umma ( TRANSPORT LICENSING (PUBLIC SERVICE VEHICLES) REGULATIONS 2017 GN. 421) hitaji la gari hizo kuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza.

Magari ya mizigo yenyewe yanaongozwa na kanuni iitwayo *Transport Licensing (Goods Carrying Vehicles) Rules, GN 390/2012. Katika kanuni hizi hakuna kipengele kinachotaka gari la mizigo kuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza. Kwa mujibu wa kanuni ya 2 gari ya mizigo ni gari lolote lililotegengezwa au limerekebishwa kwaajili ya kubeba mizigo.

Kanuni hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2017 na kanuni zinazoitwa TRANSPORT LICENSING (GOODS CARRYING VEHICLES) (AMENDMENTS) REGULATIONS 2017 GN. 420, lakini hata hivyo hakukuwa na nyongeza ya hitaji la gari kuwa na first aid kit.

Ni imani yangu makala hii itakuwa imekufungua macho zaidi kuhusu kutii sheria bila shuruti na pia kutekeleza na kusimamia sheria kwa haki na weledi. Share na mwenzako, karibu uwe balozi wa usalama barabarani.

RSAadmin1
RSA Tanzania.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote

No comments:

Post a Comment