MKOA WA SINGIDA WAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA KIPINDI CHA JULAI, 2021 HADI DISEMBA, 2021 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 24 January 2022

MKOA WA SINGIDA WAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA KIPINDI CHA JULAI, 2021 HADI DISEMBA, 2021

Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Disemba, 2021 kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa katika kikao kilichofanyika mkoani hapa mwishoni mwa wiki.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba (wa pili kutoka kushoto akiwa na viongozi wengine meza kuu wakati wa kikao hicho. Kutoka kushoto  ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Shee, Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Singida Yohana Msita .
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba akizungumza kwenye kikao hicho.


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Manyoni,  Melkizedek Oscar Humbe, Mkurugenzi wa Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkalama Asia  Messos.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Shee, akizungumza kwenye kikao hicho.



Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Singida Yohana Msita akichangia jambo kwenye kikao hicho.


Wakuu wa Wilaya wakipitia taarifa hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Selemani Mwenda, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.

Wajumbe wa Sekretariet ya Mkoa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.

Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba Ephrahim Kolimba   akipitia taarifa hiyo.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Mkoa kutoka Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye kikao hicho.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Mkoa wa Singida kutoka Wilaya ya Manyoni wakiwa kwenye kikao hicho.

Wakuu wa Idara mbalimbali za Serikali Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kutoka Wilaya ya Iramba wakiwa kwenye kikao hicho.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kutoka Wilaya ya Singida wakiwa kwenye kikao hicho.

Taswira ya kikao hicho   wakati wa kupokea taarifa hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa na Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu wakipitia taarifa hiyo.


Kikao kikiendelea.

Mbunge wa Iramba Mashariki Francis Isack akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Manyoni, Said Abdallah akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea

.
Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kutoka Wilaya ya Mkalama, Mabruki  Ng'ui akichangia jambo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga  akizungumza kwenye kikao hicho.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Yahaya Masere akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail Makhanda akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Nyalandu akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANRODS) m Mkoa wa Singida, Mhandisi Matari Masige akijibu maswali ya wajumbe katika kikao hicho.

Wajumbe wakiserebuka baada ya kikao hicho kumalizika. Wa kwanza kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Sngida Ahmed Kaburu.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge amesema pato la taifa la mkoa huo limekuwa kutoka Sh.Trilioni 2.6 mwaka 2019 hadi kufikia Sh.Trilioni 2.7 mwaka 2020 ambapo makadirio ya Mwaka 2021 yakisubiriwa.

Dk. Mahenge aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi 
(CCM) kwa kipindi cha Julai,2021 hadi Disemba, 2021 katika kikao kilichofanyika mkoani hapa mwishoni mwa wiki ambapona alimshuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizotokana tozo za miala ya simu na fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa shule, Hospitali na miradi mingine.

Mahenge alisema bajeti ya mkoa imeongeza kutoka Sh. 175,619,858,500 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Sh. 199,477,049,200 mwaka 2021/2022, Mkoa pia umepokea Fedha nje ya bajeti ilioidhinishwa na kufikia Sh. 222,188,872,239 na kuwa pato la wastani la kila mtu kwa Mkoa wa Singida limekuwa 
kutoka Sh 1,575,537 mwaka 2019 hadi kufikia shilingi 1,622,891 mwaka 2020.

UWEZESHAJI KIUCHUMI 

Akizungumzia uwezeshaji kiuchumi kutoka fedha za mapato ya ndani ya asilimia 10 alisema Jumla ya 
Sh.410, 849,769 kati ya Sh. 649,295,018 zilitolewa kwa vikundi 90 vya vijana, wanawake na watu 
wenye ulemavu sawa na asilimia 63 kwa vikundi vya vijana 31 vilipata mkopo wa  jumla ya Sh. 156,385,930, Vikundi vya Wanawake 50 vilipata jumla ya Sh.221,812,967, Vikundi vya Watu wenye 
ulemavu 9 vilipata jumla ya Sh. 32,650,873.

KILIMO

Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2020/21 Dk. Mahenge alisema Mkoa ulizalisha Tani 821,881.7 za 
mazao ya chakula kati ya lengo la kuzalisha Tani 1,103,428.6 sawa na asilimia 74.5 na mazao ya Biashara yalizalishwa tani 262,293.7 kati ya lengo la kuzalisha tani 411,599.6 sawa na asilimia 
64.

Alisema mazao ya kipaumbele ya chakula yalikuwa ni mahindi ambapo tani 382,778.9 zilizalishwa 
sawa na asilimia  81.2 ya lengo la kuzalisha tani 471,500, tani 142,786.5 za Mtama zilizalishwa sawa na asilimia  79.1  ya lengo la kuzalisha tani 180,565.1, tani 58,497.4 za Uwele zilizalishwa sawa na asilimia  64.3  ya lengo la kuzalisha tani 91,005.6, tani 34,124.5 za mhogo zilizalishwa 

sawa na asilimia  53.5  ya lengo la kuzalisha tani 63,734.9, tani 160,184.5 za viazi vitamu zilizalishwa sawa na asilimia  76.8  ya lengo la kuzalisha tani 208,588.6.


MAZAO YAKIPAUMBELE YA BIASHARA

Aklizungumzia mazao ya kipaumbele ya biashara alisema tani 148,589.8 za alizeti zilizalishwa sawa 
na asilimia  55 ya lengo la kuzalisha tani 271,745.0,tani 5,781.5 za pamba zilizalishwa sawa na asilimia  26.6 ya lengo la kuzalisha tani 21,752.4 • Tani 6,297.6 za ufuta zilizalishwa sawa na 
asilimia  58  ya lengo la kuzalisha tani 10,853.3, tani 57,655.9 za vitunguu  zilizalishwa sawa 
na asilimia  22.5  ya lengo la kuzalisha tani 256,531.6.

Aidha Mahenge alisema tani 8,084.6 za choroko zilizalishwa sawa na asilimia 67 ya lengo la kuzalisha tani 12,057.9 na kuwa tani 10,315.9 za dengu zilizalishwa sawa na asilimia 74 ya lengo la kuzalisha tani 13,933.2.


MAZAO YA KIMKAKATI 

Akizungumzia zao la kimkakati la korosho alisema Jumla ya lita 430 za viuatilifu vya zao la hilo aina ya duduba vimepokelewa kutoka Bodi ya korosho na kusambazwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya 
kuthibiti wadudu waharibifu wa zao hilo na jumla ya miche ya Korosho 492,769 inatarajiwa kuzalishwa na kusambazwa kwa wakulima wa Halmashauri kwa ajili ya msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022.
 alisema mkoa unaendelea kushughulikia malalamiko ya mashamba ya wadau mbalimbali kuhusiana na mashamba ya korosho Manyoni.

Alisema tani 145,915.8 za zao la alizeti zilizalishwa sawa na asilimia 53.7 ya lengo la kuzalisha tani 271,745.0 ambapo jumla ya tani 469.114 zenye thamani ya Sh. 3,283,798,000 za mbegu za alizeti aina ya Record zimepokelewa kutoka Serikalini kwa ajili ya wakulima kubwa,wadogo,wasindikaji wa zao hilo,mashamba ya pamoja na taasisi za Serikali magereza na mashule na kuwa mbegu hizo zilitolewa kwa ruzuku ya serikali na hivyo wakulima watalipa nusu ya bei.

Alisema jumla ya kilo 738  za mbegu za alizeti aina ya Record zimepokelewa kutoka Serikalini na kusambazwa kwenye Halmashauri kwa mchanganuo wa kilo  632 kwa ajili ya mashamba ya mfano ya maafisa ugani na kilo 106  kwa ajili ya mashamba darasa ya wakulima.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI


Akielezea kilimo cha alisema ulifanyika ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya 
Chikuyu na Mtiwe katika Halmashauri ya Manyoni kwa kurejesha mto kwenye mkondo wake kwa kujenga ukuta uliopasuliwa na mafuriko kipindi cha masika na kusababisha maji yanayoelekea kwenye skimu hiyo kuhama ambapo jumla ya shilingi 80,000,000/= zimetumika hadi sasa.


MIFUGO 

Akizungumzia suala la mifugo alisema jumla ya lita 156 za dawa aina ya Paranex zenye Ruzuku ya 
Serikali zilipokelewa kwa ajili ya kampeni ya kuogesha mifugo, jumla ya ng’ombe 606,550 mbuzi 
177,005 kondoo 80,382 na mbwa 5,385 waliogeshwa ili kujikinga na magonjwa yaenezwayo na kupe na wadudu wengine.
 

MISITU NA MALIASILI

Kwenye sekta ya misitu Dk. Mahenge alisema mkoa una hekta 433,247.48 za misitu inayojumuisha 
misitu ya Mgori (hekta 39,000), Minyughe (hekta 230,000), Mlilii hekta (5,700), Sekenke/Tulya 
(hekta 30,360) na misitu ya wananchi (hekta 128,187.48). Utekelezaji wa Shughuli na kuwa doria 16 
zilifanyika ndani ya msitu wa Minyughe ambapo wahalifu 40 walibainika na kutozwa faini.


MADINI

Katika sekta ya madini Dk. Mahenge alisema leseni za uchimbaji mdogo wa madini 103 zimetolewa 
katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Desemba, 2021 kwa wawekezaji binafsi na kutolewa mafunzo 
mbalimbali kwa wachimbaji wadogo katika wilaya za Manyoni-30, Singida Mc 45, Itigi-35.

Alitaja idadi ya wachimbaji wadogo waliopatiwa elimu ya Ijue Sheria ya Madini kuwa walikuwa 200 
Iramba-73, Ikungi 57, Singida DC-33, Manyoni na Itigi-37.

Alisema wachimbaji wadogo waliopatiwa mafunzo ya jinsi ya uchukuaji wa Sampuli za Madini walikuwa 130 Manyoni na Itigi -11, Singida DC 13, Iramba 89 na Ikungi-17.

Aidha Mahenge alisema Maduhuli ya Serikali yalikusanywa katika mauzo na makusanyo ya madini 
mbalimbali kwenye masoko ambapo kilo 239.39 ziliuzwa kwa thamani ya shilingi 27,406,699,211.66 na Mrabaha Sh.1,644,401,952.69.


BIASHARA 


Akizungumzia shughuli za viwanda na biashara alisema zimeratibiwa kwa kutoa vitabu vya leseni za 
biashara kutoka Ofisi za BRELA kwenda kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo jumla ya leseni za biashara 2,865 zimetolewa kwa wafanyabiashara Manyoni 387, Itigi-258, Ikungi248, Mkalama 292, Singida DC 96, Iramba 329 na Singida MC 1,255.

Alisema jumla ya vitambulisho 909 vya wafanyabiashara wadogo vimetolewa sawa na Sh.18,180,000
kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Disemba, 2021 ambapo Singida Manispaa 384, Singida vijijini 37, 
Manyoni 109, Itigi 25, Ikungi 94 Iramba 36 na Mkalama 224.


VYAMA VYA USHIRIKA

Kuhusu vyama vya ushirika alisema viliunganishwa vyama 25 na asasi za kifedha ambapo mikopo ya ya Sh. 1,044,200,500.00 ilipatikana kutoka kwenye taasisi za SELF, TADB, NMB, CRDB ambayo ilisaidia kujenga uwezo wa vyama vya mazao mchanganyiko vya Pamba na Tumbaku 95 kati ya 127 na kuunganishwa na masoko rasmi na vikundi vitano 5 vya vijana na wanawake vimehamasishwa ili viweze kuanzisha vyama vya pamoja vya Msingi na vyama vya akiba na Mikopo.

MAZINGIRA


Akizungumzia Mazingira Dk. Mahenge alisema udhibiti wa taka ngumu umefanyika kwa wastani wa tani 6000 hadi tani 7000 za taka ngumu na takamaji kutoka kwenye makazi ya watu, sehemu za biashara na viwandani na kuwa jumla ya kamati za mazingira 20 zimepatiwa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kuimarisha kamati za mazingira na jamii katika ngazi za kata na mitaa kuendelea kusimamia utekelezaji katika maeneo yao. • Zoezi la Uhamasishaji wa upandaji miti limeanza


ARDHI

Katika suala la vipande vya ardhi 3,008 vimepimwa kati ya lengo la kupima vipande 5,560 sawa na 
utekelezaji wa asilimia 54 na hati miliki za ardhi 769 zimetolewa kati ya lengo la kutoa hatimiliki 7,500 kwa wananchi walioomba nyaraka za umiliki wa maeneo yao sawa na utekelezaji wa 
asilimia 10.

Alisema Migogoro ya ardhi 108 imetatuliwa katika Mkoa wa Singida kati ya lengo la kutatua migogoro 165 sawa na utekelezaji wa asilimia 65.4  na kuwa Hatimiliki za kimila 6,524 zimetolewa kati ya lengo la kutoa hatimiliki za kimila 25,000 kwa wananchi walioomba kurasimisha maeneo yao sawa na utekelezaji wa asilimia 26.

Alisema Vijiji vitano (5) vimeandaa mpango wa kina wa matumizi bora ya ardhi kati ya lengo la vijiji 19 sawa na utekelezaji wa asilimia 26.3.


MIUNDOMBINU


Akizungumzia Barabara za Tanroas alisema katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya Sh. 19,718,817,000.00 zilitengwa kwa ajili ya Matengenezo ya barabara na kazi ya kuzifanyia ukarabati 
ilikuwa ni Sh. 17,704,820,000 na kulipa madeni ya wakandarasi Sh. 2,013,997,000.

 Alisema jumla ya Sh. 6,662,440,000 zimetolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, vipindi maalum, sehemu korofi, matengenezo makubwa ya madaraja na matengenezo ya kinga za madaraja katika barabara kuu na barabara za mkoa.

Akielezea matengenezo ya kawaida barabara za mkoa katika Vijiji vya Sepuka-Mlandara-Mgungira 
yamefikia asilimia 38.9, Ulemo – Gumanga- Sibiti yamefikia asilimia 12.7, ilongero – Mtinko – 
Nduguti yamefikia asilimia 9.6, Njuki – Ilongero – Ngamu yamefikia asilimia 29.3, Sabasaba – 
Sepuka- Ndago- Kizaga yamefikia asilimia 42.4, Ikungi- Londoni – Kilimatinde(Solya) yamefikia 
asilimia 43.5,Iyumbu-Mgungira-Mtunduru- Magereza(Sgd) yamefikia asilimia 29.8.

Alisema matengenezo ya vipindi maalum barabara za mkoa  Sepuka-Mlandara-Mgungira yamefikia 
asilimia 10.1 – Sabasaba – Sepuka- Ndago- Kizaga yamefikia asilimia 39.5 – Ikungi- Londoni – Kilimatinde (Solya) yamefikia asilimia 18.3 – Iyumbu-Mgungira-Mtunduru- Magereza(Sgd) yamefikia 
asilimia 74.2.

Alisema jumla ya sh. 6,293,688.000 zimetolewa kutekeleza miradi midogo ya maendeleo ya ujenzi wa 
Daraja la Msingi (mita 100) na maingilio yake (Approach Roads) ya lami yenye urefu wa km 1 
umefikia asilimia 80.

Aliongeza kuwa upanuzi wa daraja la Kilondahatari katika barabara ya Mkoa (Misigiri – Kiomboi) (mita 42) umefikia asilimia 97. ?Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Barabara ya Sabasaba – Sepuka – Ndago – Kizaga (Km 77.6) umekamilika.

Dk. Mahenge alisema kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Mchepuo ya Singida (Singida Bypass) (Km 46) umefikia asilimia 87.


UTEKELEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA KITAIFA

Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Rungwa – Itigi – Mkiwa (km 219) utekelezaji upo hatua za 
mwisho za manunuzi, Ukarabati wa barabara ya Singida – Shelui (Km 110) utekelezaji upo kwenye 
hatua ya maandalizi ya kufanya upembuzi yakinifu, Ujenzi wa barabara ya Handeni-Kibereshi-
ChembaSingida (Km 460) utekelezaji umeanzia Handeni mkoani Tanga, Ujenzi wa barabara ya Karatu-
Mbulu-Haydom-SibitiLalago-Maswa (Serengeti by Pass) utekelezaji utaanzia Mbulu-Hydom.

Alisema ujenzi wa Kituo cha ukaguzi wa Magari (OSIS) eneo la Muhalala – Manyoni, utekelezaji upo 
kwenye hatua za kisheria za kumuondoa Mkandarasi aliyepo kutokana na kukiuka taratibu za imkataba. ?Ujenzi wa daraja la Sibiti (Mita 82), Serikali imetenga sh. 2,500,000,000 kujenga km 25 kwa kiwango cha lami. ?Ujenzi wa daraja la Sanza (Mita 75) utekelezaji unasubili kibali kwa ajili ya kuanza mchakato wa manunuzi wa kumpata Mkandarasi.

Akielezea Barabara za Tarura Dk. Mahenge alisema jumla ya Sh. 3,629,200,198.65 zimetolewa kwa 
ajili ya kufanya matengenezo ya aina mbalimbali kwenye barabara za mijini na vijijini na vivuko
mchanganyiko. 

NISHATI – UMEME 

Dk. Mahenge akizungumzia nishati ya Umeme alisema mahitaji ya umeme kwa wakazi wa mkoa wa Singida ni Wastani wa Megawati 10, ambapo uwezo wa upatikanaji wa umeme ni Megawati 232, hali hii imefanya mkoa kuwa na ziada ya Megawati 222 na kuwa Shughuli zilizotekelezwa ni jumla ya Sh. 
3,606,993,620 zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ukarabati wa laini tano za msongo wa 
kati (33 na 11KV) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 62. (jedwali na.28)

Alisema jumla ya Sh. 31,900,628,901.06 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa REA III 
Round 2 katika Halmashauri za Wilaya ya Ikungi na Singida ambapo usanifu wa kina, upembuzi 
yakinifu na manunuzi ya vifaa (waya, nguzo na transformer) umefanyika pamoja na usambazaji na 
usimikaji wa nguzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Alisema kuwa jumla ya Sh. 28,000,000,000 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa REA III 
Round 2 katika Halmashauri za Wilaya ya Iramba, Mkalama na Manyoni ambapo usanifu wa kina na 
upembuzi yakinifu unaendelea kufanyika.


CHANGAMOTO ZA UMEME NA HATUA ZA UTATUZI (MKALAMA & IRAMBA) 

Alisema mkoa umeweka mkakati wa makusudi wa kupitia laini yote ya Umeme nguzo kwa nguzo ili kubainisha matatizo yote na kuyarekebisha, kikosi kazi kimeanza kazi tangu tarehe 19.01.2022


HUDUMA ZA KIJAMII


Akizungumzia sekta ya elimu hasa sehemu ya ufaulu alisema darasa la Saba watahiniwa 35,573 wanaume walikuwa 16,677 na wakike-18,796 na walifanya mtihani wa kuhitimu D.7 (PSLE-2021) ambapo watahiniwa 28,072 wakiume 13,054 na wa kike 15,018 walifaulu mtihani huo sawa na asilimia 78.91.
  

UTEKELEZAJI WA MIRADI – MIRADI YA UVIKO 19 

Akielezea Ujenzi wa vyumba vya madarasa 330 kwa shule za sekondari na 332 kwa shule za msingi na
Mabweni mawili kwa shule za msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu umefanyika kupitia 
mpango wa UVIKO 19 kwa gharama ya Sh. 13,400,000,000.

Alisema jumla Sh. 275,000,000 ya fedha za Tozo ya miamala ya simu zilitolewa kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya madarasa ambapo utekelezaji upo hatua mbalimbali za ukamilishaji. 


MIRADI YA AFYA – FEDHA ZA UVIKO HALMASHAURI KITUO


Akizungumzia miradi ya fedha za Uviko zilizotumika wilayani Ikungi ni ujenzi wa jengo la dharura 
(EMD) ICU nyumba ya watumishi (3 IN ONE) Hospitali ya Wilaya kwa  gharama ya Sh.90,000,000 
90,000,000.

Alisema Iramba DC Hospitali ya Wilaya ya Iramba Sh.300,000,000 250,000,000 90,000,000 640,000,000 Itigi DC Kituo cha Afya Rungwa,Sh. 90,000,000 90,000,000, Manyoni DC Hospitali ya Wilaya Manyoni Sh.300,000,000 90,000,000 390,000,000, Mkalama DC Hospitali ya Wilaya Mkalama Sh.300,000,000 90,000,000 390,000,000, Singida DC Hospitali ya Wilaya Singida Sh.250,000,000 90,000,000 340,000,000 jumla ikiwa ni Sh.1,940,000,000.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba alisema Serikali imetoa Sh.1,915,815,144.43 ikiwa 
ni fedha za ruzuku kwa ajili ya kununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa kipindi cha Mwaka 
2020/21 ambapo imewezesha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ashiria
(Tracer medicines) kufikia wastani wa asilimia 94.2 Mwezi Desemba 2021 kwa kila Halmashauri.

Alisema hadi kufikia Desema 31/2021 mkoa ulikuwa umeshachanja wateja 50,913 chanjo dhidi ya 
UVIKO-19 (chanjo aina ya Janssen wateja 26,739, chanjo aina ya sinopharm 20,396 na chanjo aina ya 
Pfizer wateja 3,778).


MAJI 

Kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Singida alisema ni asilimia 75 kwa wananchi
wa Mjini na Asilimia 57.9 kwa wananchi wa vijijini, aidha Jumla ya vijiji 303 vinapata huduma ya 
maji katika Mkoa wa Singida.

Alisema jumla ya Sh. 7,671,576,435.38 zimetolewa kutekeleza miradi ya Maji katika Mkoa wa Singida 
kati ya lengo la Bajeti ya Sh. 12,363,350,455.89 (Jedwali na.40) ?Ujenzi wa Miradi nane (8) ya 
Maji imekamilika na inatoa huduma.

Alisema ujenzi wa Miradi mitatu (3) ya Maji (Kisiriri, Zinziligi na Maluga – Iramba) imefikia asilimia 85, ujnzi wa Mradi mmoja (1) wa Maji ( Ughandi B – Singida DC) umefikia asilimia 75. 

Akielezea utekelezaji wa Miradi ya UVIKO 19 jumla ya Sh 4,046,043,493.00 zimetolewa kutekeleza 
Miradi tisa (9) ya Maji ambayo itatekelezwa kwa miezi sita na ikikamilika itahudumia wananchi 
45,764 wa Mkoa wa Singida na kuwa wakandarasi wamepatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji.


UTAWALA BORA  NA VIKAO VYA KISHERIA 


Dk. Mahenge alisema vikao vya Mabaraza ya Halmashauri 8 kati ya 7 vimefanyika sawa na asilimia 
114.3  za utekelezaji, vikao ngazi ya Kata (WDC’s) 117 kati ya 136 vimefanyika sawa na asilimia 
86 za utekelezaji, mikutano mikuu ya Vijiji 288 kati ya 441 imefanyika sawa na asilimia 65.3 za 
utekelezaji, mikutano ya Wakazi wa Mitaa 14 kati ya 53 imefanyika sawa na asilimia 26.4 za 
utekelezaji, na jumla ya vikao 2 vya Mabaraza ya wafanyakazi vimefanyika kwenye Halmashauri. 


WAFANYAKAZI

Kuhusu Utawala bora alisema jumla ya watumishi 265 waliajiriwa na kupangiwa kazi katika Mkoa wa 
Singida wakiwepo walimu wa shule za msingi 92, Walimu wa Shule za Sekondari 80 Watumishi wa Afya 86 na watumishi wa kada nyingine.


MAZINGIRA YA KUFANYIA KAZI NA MAKAZI – MAJENGO


Akizungumzia mazingira ya kufanyia kazi alisema jmla ya Sh. 1,000,000,000 zimepokelewa 
kuendelea na ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Singida awamu ya pili na jumla ya Sh.
443,285,117.46 zimepokelewa kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya 
Mkalama, jumla ya Sh. 150,000,000 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba tatu za watumishi 
Halmashauri ya Wilaya ya Singida.


SERIKALI ZA MITAA 

Kuhusu Serikali za Mitaa alisema kumekuwa na ongezeko la makisio ya Bajeti ya Mapato ya ndani kutoka Sh.15,634,787,195 Mwaka 2020/2021 hadi kufikia Sh.16,881,647,581 Mwaka 2021/2022 na kuwa jumla ya Sh. 8,317,996,497.77 zimekusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Singida kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Disemba 2022 sawa na utekelezaji wa asilimia 49 za lengo la kukusanya  Sh. 16,881,647,581 kwa mwaka 2021/2022.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba alitumia kikao hicho kumpongeza Dk.Tulia Ackson kwa kupitishwa na chama hicho kugombea Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa ni dalili njema ya kupata mwakilishi atakaye peperusha vema bendera kwa kulinda maslahi mapana ya nchi na mhimili wa Bunge.

Kilimba amewaomba wabunge wote wa CCM na hasa wa Singida kuungana na wenzao na kumchagua kwa kuwa CCM Singida inaimani naye kutokana na uzowefu alio nao. 

No comments:

Post a Comment