Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mbeya, Decemba 1, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). |
*Asema kauli, vitendo na mitazamo ya ubaguzi kwa kundi hilo havikubaliki
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka husika kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kuwanyanyapaa na kuwabagua Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) kwa kuwa vitendo, kauli au mitazamo ya unyanyapaa na ubaguzi kwa kundi hilo havikubaliki.
“Kumekuwa na madai kuwa watumishi wa afya wana tabia za unyanyapaa na kuvujisha siri za WAVIU wanapotoa huduma katika vituo vyetu vya tiba na matunzo kwa WAVIU. Vitendo na tabia hizi ziripotiwe mara moja pindi vitakapotokea.”
Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Desemba Mosi, 2021) wakati alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe mkoani Mbeya. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Zingatia Usawa. Tokomeza Ukimwi. Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko.”
Mheshimiwa Majaliwa amesema nchi ina sheria ya UKIMWI ambayo imefanyiwa marekebisho kadhaa ili kuhakikisha kuwa huduma za VVU na UKIMWI zinamfikia kila mlengwa. “Ninaelewa kuwa unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU bado ni changamoto kubwa katika jamii zetu.”
No comments:
Post a Comment