WADAU WA SANAA WAIPONGEZA SERIKALI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 24 November 2021

WADAU WA SANAA WAIPONGEZA SERIKALI

Miss Tanzania 2020/ 2021 Rose Manfere.

NA ADELADIUS MAKWEGA, DSM

WADAU kadhaa wa Utamaduni Sanaa na Michezo wa lioshiriki katika hafla ya mambo makubwa sita ya WUSM iliyofanyika Dar es Salaam Novemba 22, 2021 wametoa pongezi kwa serikali namna inavyoshirikisha wadau wake katika shughuli za kiserikali huku wakiomba moyo huo kuendelea ili kujenga umoja wa taifa letu

Akizungumza katika hafla hiyo, wakwazwa kukipiga kipenga cha pongezi alikuwa ni Steve Nyerere ambaye amesema kuwa namna Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyoendesha nchi ni sawa na refa anayeuchezesha mchezo vizuri bara na visiwani.

“Ohh mama anaupigwa mwingi mimi nasema kweli anaupiga mwingi katika utulivu na amani taifa letu. Sasa nchi yetu ni shwari”

Pia msanii huyu wa filamu na uchekeshaji ameipongeza WUSM na michezo tangu Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kwa ushirikiano wao kwa wasanii wote. “Dkt Hassan Abbasi amekuwa akitupgia simu kuna wakati hadi usiku akisisitiza ushiriki wetu katika shughuli hizi za kiserikali na hakika sisi lazima tunawaunga mkono.”

Pongezi za pili kwa serikali zilitoka kwa Miss Tanzania 2020/ 2021 Rose Manfere alisema kuwa hata wao warembo sasa tunakumbukwa ipasavyo. Kwani ushiriki wa  warembo katika kazi za serikali unaonekana wazi mathalani uteuzi wa Balozi Hoyce Temu na Basila Munukuzi katika ukuu wa wilaya unaonesha picha nzuri ya Rais Samia kwa wadau wa Sanaa.

“Ushirikianoa huu uwe manufaa kwa utamaduni wetu, Sanaa  yetu na hata Michezo yetu.”

 Aliongeza salaam za pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan na WUSM

Salaam hizo za pongezi zilitolewa na wasanii na wadau mbalimbali wa Sanaa, utamaduni na Michezo wakati walipopewa nafasi ya kutoa salaam zao mara baada ya Waziri Innocent Bashungwa kuzindua Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, kuanza kwa mashindano ya Samia Taifa CUP na kuzindua mifumo ya kidigitali ya taasisi zilzo chini ya wizara hii.


No comments:

Post a Comment