KAMPUNI ya UTT AMIS ikiwa ni mdau mkubwa wa Usalama Barabarani imedhamini
Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa jijini Arusha.
Inawakumbusha wawekezaji wake na watanazania wote kwa ujumla kujali usalama wao wawapo barabarani na kujali usalama wa wengine.
Sambamba na udhamini huo UTT AMIS inashiriki maonyesho yanayoambatana na maadhimisho hayo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UTT
AMIS inawakaribisha wakazi wa Arusha kutembelea banda lao ili kujifunza
juu ya uwekezaji wenye tija kwenye mifuko inayosimamiwa na UTT AMIS. Maadhimisho hayo yameanza rasmi Novemba 23 na yatafikia kilele chake Novemba 28.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza Novemba 23-28 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Wananchi wakimsikiliza Afisa Uendeshaji wa Kampuni ya UTT AMIS, Hilder Lyimo wakati akiwaelezea fursa zinazopatikana katika kampuni hiyo.
Afisa Uendeshaji UTT AMIS ofisi ya Arusha, Wishiko Makumbati, akitoa maelezo kuhusu faida na fursa zinazopatikana katika mifuko inayosimamiwa na UTT AMIS.
No comments:
Post a Comment