Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo akiwa na afisa mahusiano ya jamii Wiston Kandamo wakiwa kwenye moja ya mawadati yaliyotolewa na Asasi ya Kiraia ya Utafiti na Uhifadhi wa wanyamapori ya Lion Landscapes.
Na Fredy Mgunda, Iringa
KAYA 138 za vijiji vitatu vya tarafa ya Pawaga Wilayani Iringa zimekabidhiwa kadi za Bima ya Afya zilizotolewa na Asasi ya Kiraia ya Utafiti na Uhifadhi wa wanyamapori ya Lion Landscapes kwa lengo la kuwarahisishia matibabu.
Kaya hizo ni kutoka kijiji cha Kinyika, Isele na Kisanga ambapo kando ya Bima hizo, vijiji hivyo vimepokea msaada wa Madawati ya shule za msingi na chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi za vijiji hivyo, huku wafugaji wakipokea dawa ya mifugo,huku timu za mpira wa miguu wakipewa mipira miwili miwili na msaada huo umegharimu sh.15 milioni.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo afisa mahusiano ya jamii Wiston Kandamo alisema kuwa zawadi hizo zimetokana na kila kijiji kutengwa kamera tatu ambazo zinatumika kuwapiga picha wanyamapori wanaopita katika maeneo ambayo kamera zimetegwa.
Kandamo alisema kuwa kwa msindi wa kwanza kupiga picha wanyama wengi hujipatia kiasi cha shilingi milioni 4 kwa mshindi wa kwanza ,mshindi wa pili anapata kiasi cha shilingi milioni 3 na mshindi wa tatu anapata kiasi cha shilingi milioni 2 na zoezi hilo hufanyika kila baada ya miezi mitatu.
Alisema kuwa fedha hizo hutumika kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu,afya na sekta ya mifugo ambapo kila sekta hutaja mahitaji ambayo wanayoyahitaji kwa kijiji kwa mujibu wa vikao husika.
Kandamo alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha wananchi wanajua umuhimu wa kuwatunza wanyama pori ambao wanawazunguka kwenye vijiji vyao na kuwalinda wasitoweke kwa kujua umuhimu wa kupata faida kutokana na wanyama hao.
Aliongeza kuwa mradi huo umekuwa na manufaa kadhaa ikiwepo baadhi ya makabili kuanza kubadili mira zao hasa kwa kuacha kuwawinda wanyama aina ya pata ambao wamekuwa wakiua na kula mifugo yao,hivyo uwindaji wa kimira kwa makabila ya wamasai na wabarabait wameacha kabisa tabia hiyo katika maendeo ambayo mradi unafanya kazi.
Kandamo alisema kuwa moja ya changamoto ambayo wamekuwa wanakabiliana ni baadhi ya wananchi kuiba kamera au kuharibu kabisa katika maeneo ambayo zimetegwa hivyo wananchi wanarudisha nyuma jitihada za kuwalinda na kuwatunza wanyama pori.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akizungumza na wanufaika wa msaada huo amewahimiza kuboresha mahusiano na Taasisi za Uhifadhi wa wanyamapori ili kuendelea kunufaika na matunda yatokanayo na uhifadhi.
Moyo alisema kuwa serikali ya wilaya inawashukuru kwa kazi kubwa wanayoifanya Asasi ya Kiraia ya Utafiti na Uhifadhi wa wanyamapori ya Lion Landscapes kwa kuboresha maendeleo ya wananchi na kuwalinda wanyamapori ambao wapo hatarini kupotea.
Alisema msaada ambao unatolewa na Asasi ya Kiraia ya Utafiti na Uhifadhi wa wanyamapori ya Lion Landscapes unatija kubwa kwa wananchi wa vijiji husika kimaendeleo na kuinua uchumi wao.
Moyo alitoa onyo kwa wananchi wote ambao wanajihusisha na uharibifu na wizi wa kamera ambazo zinakuwa zimetegwa kwenye vijiji husika watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa watu hao wanakuwa wanahujumu uchumi wa kijiji.
Alisema kuwa mradi unatekelezwa na Asasi ya Kiraia ya Utafiti na Uhifadhi wa wanyamapori ya Lion Landscapes ni muhimu sana kwa maendeleo wa vijiji husika kwa kuwa unalenga kukuza uchumi wa wananchi.
Miongoni mwa waananchi wameishukuru Asasi ya Lion Landscapes kwa kuendelea kuviwezesha kimaendeleo vijiji vya pembezoni mwa Hifadhi ya Ruaha na kueleza kuwa miongoni mwa mafufaa pamoja na kusaidiwa katika ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa katika shule za msingi.
No comments:
Post a Comment