Wachezaji wa timu ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam wakifurahi baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Kitaifa wa mashindano ya CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa kuwashinda timu ya Mkoa wa Arusha katika fainali.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi (katikati) akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ,Omari Juma (kulia) mara baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Kitaifa wa CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofanyika Jijini Dodoma ,kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB , Abdulmajidi Nsekela.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Deogratius Ndejembi (katikati) akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya mpira wa kikapu wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Hadija Kalambo (kulia) mara baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Kitaifa wa CRDB Taifa Cup 2021 yaliyofanyika Jijini Dodoma ,kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,Abdulmajidi Nsekela.
Mfungaji bora wa Kiume kutoka Timu ya kikapu ya Mkoa wa Arusha, Tyrone Edward akikabidhiwa kombe lake.
Mashabiki wakifuatilia Michezo ya fainali.
Timu ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (jezi Nyeusi) wakichuana na wenzao wa Arusha. Dar ikishinda kwa 71-52.
Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam (Blue Bahati) wakichuana na Timu ya Kikapu Unguja. Dar ikishinda 67 - 55.
*****
Na Mwandishi wetu, DodomaTIMU za mpira wa kikapu za kiume na wanawake za mkoa wa Dar es Salaam zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya CRDB Benki Taifa Cup kwa mwaka huu.
Wakati timu ya wanawake ya Dar es Salaam ikitwaa taji hilo kwa kuifunga Unguja kwa pointi 67-55, wanaume ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa kuwachabanga Arusha kwa pointi 71-52. Michezo hiyo ilifanyikia kwenye viwanja vya Chinangali, Dodoma.
Washindi hao walikabidhiwa makombe yao na Naibu waziri, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Mbali ya vikombe, washindi pia walikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 6.5 milioni kwa washindi wa kwanza huku washindi wa pili wakikabidhiwa hundi ya Sh3 milioni kila mmoja.
Pia kulikuwa na zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na ile ya mchezaji mwenye thamani kubwa MVP ambapo Alinani Endrew wa Dar es Salaam alishinda kwa upande wa wanaume na Noela Renatus pia wa Dar es Salaam alishinda kwa uoande wa wanawake.
Akizungumza mara baada ya michezo ya fainali, Mkurugenzi Mteandaji wa benki ya ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema kuwa wanajisikia faraja kubwa kufanikisha mashindano hayo ambayo mpaka sasa yameleta tija na chachu ya maendeleo ya mpira wa kikapu nchini Tanzania.
Benki ya CRDB imetumia Sh300 milioni kudhamini mashindano hayo. Mbali ya benki ya CRDB kuwa wadhamini wakuu, wadhamini wengine walikuwa GSM, Azam TV, Sanlam, Tulia Trust, PSSF, EFM na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Nsekela alisema kuwa mbali ya kuchangia maendeleo ya michezo kupitia mashindano hayo, benki ya CRDB imesaidia vijana kwa kutoa fursa ya za ufadhili wa masomo na kuchangia katika sekta ya elimu.
Alisema kuwa wamekuwa wakipokea salamu nyingi za pongezi kutoka wa viongozina watu mbalimbali ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa maamuzu yao ya kudhamini mashindano hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Nsekela pia alisema kuwa benki ya CRDB itaendelea kuwekeza katika mchezo wa mpira wa kikapu na kuhakikisha kuwa unakua mmoja kati ya michezo yenye kubadili maisha ya vijana kiuchumi ili kuendana na kauli mbiu yake ya “Ni Zaidi ya Game Ni Maisha”.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki ya CRDB, Dkt Ally Laay alizipongeza timu zote zilizoshiriki, wadau, mashabiki na wadhamini wengine kufanikisha mashindano hayo.
Alisema kuwa Menejimenti ya benki ya CRDB imedhamini mashindano hayo kwa kujua kuwa yana tija kwa kwani inatoa fursa kwa vijana mbali na maendeleo ya michezo nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ndejembi aliwapongeza wadhamini, wachezaji na viongozi wa timu zote 32 zilizoshiriki katika mashindano hayo ya siku 10.
Ndejembi alisema kuwa mchezo wa mpira wa kikapu una fursa nyingi mbali ya kukuza vipaji, kwani pia umewekeza katika elimu.
Hamasa imekuwa kubwa sana na kila kona ya nchi hususan hapa Dodoma watu wanazungumzia CRDB Bank Taifa Cup kuanzia masokoni, maofisini, mitaani hadi Bungeni,” alisema Ndejembi.
Alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yametoa funzo kwa wachezaji na kuwataka wasisubiri fursa za kwenda NBA na ligi nyingine kubwa kwani wanatakiwa kuzifuata huko na kuonyesha vipaji vyao.
Aliongeza kuwa idadi ya mashabiki imekuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huu na kutoa wito kwa TBF kuendeleza mchezo huu mpaka ngazi za shule za msingi na sekondari.
No comments:
Post a Comment