Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na tabasamu baada ya kukagua miradi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakizungumza mara baada ya ziara.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakikagua miradi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Mmoja ya majengo yanayojengwa katika kituo cha afya Isman ambayo kwa ujumla wake yanatakiwa kujengwa majengo matano.
Na Fredy
Mgunda, IringaMKUU wa Mkoa wa
Iringa, Queen Sendiga ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhakikisha
inasimamia vilivyo miradi inayokelezwa katika Halmashauri hiyo ili kuendana na
thamani ya fedha ambazo zinakuwa zimetolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha
huduma za jamii katika maeneo husika.
Akizungumza wakati wa
kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo, mkuu wa mkoa wa Iringa alisema
kuwa Halmashauri ya wilaya ya Iringa imebahatika kuwa na miradi mingi ya
kimaendeleo ambayo imetumia mamilioni ya fedha kutoka serikalini kuu na
serikali za mitaa kwa ajili ya kukuza maendeleo ya wananchi.
Sendiga alisema kuwa
miradi aliyoitembelea kwa siku ya leo kwa kiasi kikubwa imetekelezwa katika
ubora ambao unatakiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolea kwenye
mradi husika kama vile ujenzi wa majengo matano ya kituo cha afya cha
Ismani,ujunzi wa vyumba viwili ya shule ya sekondari ya Nyang’oro na
Lyandembela.
Alisema kuwa
amefurahishwa kwa namna ambavyo miradi yote hiyo imejengwa kwa ubora hasa
miradi ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari ya Nyang’oro na
Lyandembela na ujenzi unaondelea katika kituo cha afya cha Ismani alilidhishwa
na ubora wa vifaa vya ujenzi vinavyotumika kujengea kama vile tofali zenye
ubora unaotakiwa, saruji ilivyochanganywa kwenye ubora unaotakiwa.
Sendiga aliwapongeza
viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kusimamia vizuri miradi yote
inayotekelezwa ambayo imekuwa inaubora unaotakiwa kulinga na thamani ya fedha
ambazo zimetolewa na serikali.
Alisema kuwa uongozi
wa wilaya na halmashauri wamefanya kazi kubwa kuhakikisha miradi hiyo
inatekelezwa kwenye ubora unaotakiwa kama ambavyo serikali inataka kujengwa kwa
ajili ya kutoa huduma kwa ajili ya jamii.
Aidha sendiga alisema
kuwa hajaridhishwa na fundi aliyepewa kazi ya kutengeneza madawati ya shule ya
sekondari ya Nyang’oro chini ya kiwango na kupelekea kuharibika kabla ya kuanza
kutumika hivyo kumuamuru fundi huyo kutengeneza tena madawati hayo kwa gharama
zake.
Alimuagiza mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuhakikisha anamsimamia fundi huyo
anatengeneza madawati hayo kwenye ubora unaotakiwa kama ambavyo madawati
mengine kwenye shule hiyo yalivyotengenezwa na kudumu kwa miaka mingi.
Mkuu wa mkoa huyo
alifanikiwa kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa majengo matano ya kituo cha
afya cha Ismani na kuzindua vyumba viwili vya madarasa katika shule ya
sekondari ya Lyandembela iliyopo katika kata ya Ifunda.
Sendiga alimazia kwa
kuwapongeza viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa kufanya kazi kwa ushirikiano
mzuri na ofisi ya mkuu wa wilaya na mkoa na kusababisha kuleta matokeo chanya
kwenye miradi ambayo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Alisema kuwa
anawapongeza wananchi wote ambao wamekuwa wanajitokeza kuchangia nguvu zao
kwenye miradi yote ambayo imekuwa inayotekelezwa kwenye maeneo yao na kuipatia
nguvu serikali kuendelea kupeleka miradi kwenye halmashauri hiyo
Kwa upande wake mkuu
wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhuru Hassan ametoa kiasi cha shilingi
Milioni Mitatu (300,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura na
ametoa shilingi milioni mia nne na ishirini (420,000,000/=) kwa ajili ya mashine
ya mionzi (exrey).
Alisema kuwa
anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhuru
Hassan kwa kuwapatia fedha hizo ambazo zikifika zitafanyiwa kazi kwa haraka
sana na kwenye ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha hizo.
Moyo alisema kuwa
hata mvumia mtu yeyote yule ambaye atakuwa anaihujumu miradi ya kimaendeleo
ambayo inatekelezwa katika wilaya ya Iringa hivyo miradi yote itatekelezwa
kulingana na thamani ya fedha ambazo ambayo itakuwa imetolewa na serikali kwa
ajili ya mradi husika.
Alisema kuwa tatizo la
maji katika tafara ya Isiman litatuliwa
na mradi wa maji wa Kilolo na Isman ndio utakuwa suruhisho la kupatikana
kwa maji na kumaliza changamoto zote ambazo zinapatika na kukosekana kwa maji.
Naye mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bashir Muhoja alisema kuwa walipokea kiasi cha
shilingi milioni mia nne (400,000,00/=) kwa ajili ya majengo matano ambayo ni
jengo la Maabara, nyumba ya mtumishi wa kituo hicho, jengo la kuhifadhia maiti, jengo
la upasuaji na jengo wazazi
Alisema kuwa katika
ujenzi wa majengo hayo matano wameshatumia kiasi cha shilingi milioni mia mbili
sabini na sita (276,000,000/=) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya
viwandani kama vile saruji, malumalu, vifaa vya mbao, nondo, Gypsum Board na vifaa
vingine vinavyohitajika katika ujenzi huo.
Muhoja alisema kuwa
mradi huo umekumbana na baadhi ya changamoto kutokana na kupanda kwa gharama za
vifaa vya ujenzi sokoni kama vile vifaa vya vyuma na kusema kuwa kiasi cha shilingi
milioni mia nne (400,000,00/=) haziwezi kukamilisha kituo hicho.
Alisema kuwa fedha
iliyo inaweza kufikisha asilimia 95 na kutakosekana baadhi ya vitu
vitakosekana ambavyo vitasababisha
kutofikia lengo la kumaliza majengo hayo na kuanza kutumika kama inavyotarajiwa
na serikali.
No comments:
Post a Comment