BENKI
ya CRDB imepongezwa kwa kufanikisha kuimalika kwa ushirikiano wa
kibiashara kati ya Tanzaniana Burundi kupitia huduma zake za kibenki.
Akizungumza
jijini Dodoma siku ya Ijumaa baada ya kuweka jiwe la msingi la uijenzi
wa kiwanda cha Itracom Fertilizers Limited cha wawekezaji kutoka
Burundi, Rais Evariste Ndayishimiye alisema, benki ya CRDB imekuwa
mshirika mkubwa wa kuimalisha biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi
mbili. Benki ya CRDB imetoa mkopo wa kuwezesha ujenzi wa kiwanda hicho
cha mbolea.
“Uwezeshaji
uliofanywa na benki katika ujenzi wa kiwanda hiki cha mbolea ni
ushahidi tosha wa namna gani benki imejikitia katika kufanikisha
kuimalika kwa biashara na uwekezaji baina ya nchi zetu zenye udugu wa
karibu,” Rais Ndayishimiye alisema.
Alisema
uwekezaji huo wa raia kutoka nchini kwake, utawezesha kiwanda cha
mbolea cha Itracom kuzalisha tani laki sita kwa mwaka na kutoa ajira kwa
Watanzania wasiopungua elfu 10.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki yake yenye matawi matatu nchini Burundi imekuwa ikitoa mikopo kwa miradi mbali mbali ya kimkakati ya serikali ya Burundi na Tanzania. Benki inatarajia kufungua tawi la nne wilayani Gitega mwaka huu.
Nsekela
alisema benki yake imekuwa inafanya biashara kwa muda mrefu na
wawekezaji wa Itracom huko Burundi kwa kuwapatia huduma zote za kibenki.
Miongoni mwa miradi ambayo benki imefadhili huko Burundi ni pamoja na
ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha Fomi na kiwanda cha simenti huko Rutana
ambacho benki imetoa mkopo wa dola za Marekani milioni 10.
“Mheshimiwa Rais, umepo wako hapa leo kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda cha Itracom ni ushahidi tosha wa kuimalika kwa uhusiano baina ya Burundi na Tanzania. Kama benki ya kizalendo yenye mtazamo wa kimataifa, Benki ya CRDB ina mkakati wa maksudi wa kuwezesha kuimalika kwa mahusiano ya kibiashara na uwekezaji baina ya nchi za Afrika ya Mashariki ili kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu,” alisema.
Mkurugenzi
huyo wa Benki ya CRDB aliongeza kwamba benki hiyo imeshawekeza mtaji wa
kiasi cha dola 107 milioni nchini Burundi katika sekta mbalimbali za
uchumi wan chi hiyo ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa maji Mpanda.
Benki
hiyo pia imewezesha kampuni ya Itracom kuwekeza katika kiwanda cha
mbolea cha Minjingu kilichopo Babati mkoani Manyara. “Hapa nchini
Tanzania benki yetu imewezesha kampuni ya Itracom kwa kuipatia mkopo wa
dola 12 milion kwaajili ya ujenzi wa kiwanda cha Minjingu kilichopo
Babati,” Nsekela alisema.
Tangu
ianzishe kampuni tanzu nchini Burundi mwaka 2011, Benki ya CRDB imetoa
mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa kupitia kutoa ajira kwa Warundi na
pia kulipa kodi mbalimbali za serikali kufanikisha maendeleo.
No comments:
Post a Comment