RC SINGIDA ATEMBELEA WALIPO WAMACHINGA KUBAINI CHANGAMOTO ZAO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 September 2021

RC SINGIDA ATEMBELEA WALIPO WAMACHINGA KUBAINI CHANGAMOTO ZAO

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mhenge alipotembelea soko la nguo katika eneo la Posta Manispaa ya Singidamjini, upande wa kulia ni Afisa Biashara wa Manispa hiyo.

Dkt. Binilith Mahenge akiwa katika ziara kwenye soko la Kariakoo Manispaa ya Singida mjini.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo (kulia ) akijadiliana jambo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo  Asia Juma Messos wakati wa ziara hiyo.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko (aliyeshikakitambaa) akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo wakati wa ziara hiyo. 

Na Mwandishi Wetu, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo amefanya ziara katika masoko na mitaa ya Manispaa ya Singida ili kubaini hali halisi ya maeneo hayo na changamoto zinazo wakabili wafanyabiashara  wadogomaarufu kama wa machinga.

Ziara hiyo iliyoshirikisha Kamati ya Usalama ya mkoa na viongozi mbalimbali wa manispaa hiyo ililenga kubaini maeneo yenye changamoto kwa wafanyabiashara wenye maduka na wanaopanga bidhaa barabarani.

Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amewataka wakurungezi na wakuu wa wilaya kuhakikisha zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara hao linafanyika kwa njia  yamajadiliano badala ya kutumia nguvu.

Aidha Dkt. Mahenge amemshauri Mkurungezi wa Manispaa ya Singida mjini ashirikiane na vyombo vingine ikiwemo TARURA  ili walete mapendekezo ya maeneo tarajiwa pamoja na mipango ya namna ya utekelezaji.

Hata hivyo amebainisha kwamba maeneo tarajiwa lazima yaandaliwe vizuri ikiwemo ujenzi wavyoo, uwepo umeme na maji ili maeneo hayo ya wavutie wafanyabiashara.

Aidha amesema mchakato wa kubaini maeneo mapya ya kufanyia biashara na mipango ya kufunga baadhi y a Barabara kwa nyakati  tofautiinafanyika ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anaendelea na  shughuli zake bila kubughuziwa.

“Nashauri wafanyabiashara wa mjini ambao watatakiwa kupisha maeneo waliopo watafutiwemengine upande wa huko mjini na wafanyabiashara wa mitaani watafutiwe maeneo karibu namitaa yao.”alisema Dkt. Mahenge.

Hata hivyo amewataka wataalamu mbalimbali walio fuatana nao kutumia fursa hiyo kufanya mipango miji wakati wa kufungua maeneo mapya kwa ajili ya biashara.

Ametoa wito kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kushirikiana ili kuhakikisha zoezi la kuwapanga wafanyabiashara hao halichukui muda mrefu iwe wameshapatiwa maeneo mapyaya bisharakwa njia ya majadiliano.


No comments:

Post a Comment