MACHINGA IRINGA WAGOMA KUONDOKA ENEO LA MASHINE TATU NA MIOMBONI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 25 September 2021

MACHINGA IRINGA WAGOMA KUONDOKA ENEO LA MASHINE TATU NA MIOMBONI

 Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu akiwa sambamba na madiwani wa viti maalum manispaa ya Iringa pamoja na viongozi wa Machinga Iringa.

Madiwani wa viti maalumu(CCM) Iringa wakiwa na viongozi wa Machinga mkoa wa Iringa wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu wakati akiongea na machinga wa Manispaa ya Iringa.

Baadhi ya wafanyabishara wadogowadogo waliojitokeza kumsikiliza mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu wakiwa na mabango yao.

Baadhi ya wafanyabishara wadogowadogo waliojitokeza kumsikiliza mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu


Na Fredy Mgunda, Iringa

WAFANYABIASHARA wadogo wadogo wa Manispaa ya Iringa (Machinga) wamesema kuwa hawapo tayari kuondoka katika eneo la Mashine Tatu na Miomboni kwa kuwa maeneo hayo ndio ambayo yanawateja wengi wanaonunua bidhaa kwa wingi tofauti na maeneo mengine.

Wakizungumza kwenye mkutano waliofanya na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu walisema kuwa wanaheshimu na kufuata maagizo yote ya Waziri Mkuu Pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa machinga wapangwe vizuri na sio kuondoshwa kwenye maeneo yao.

Walisema kuwa eneo la Mashine Tatu wamekuwa wakifanyia biashara zao kwa miaka mingi na limezoeleka kwa wanunuzi wengi kwenda kununua bidhaa ndogo ndogo katika eneo hilo inakuaje sasa wanataka kuwaondoa katika eneo hilo la kibiashara ambalo wao ndio wamelitengeneza kwa kiasi kikubwa.

Wachinga hao waliongeza kwa kusema kuwa hawapo tayari kuondoka na hawezi kuondoka katika eneo hilo ambalo limekuwa linamzunguko mkubwa wa biashara tofauti na maeneo mengine ambayo inasemekana Serikali ya halmashauri ya manispaa ya Iringa imepanga kuwapeleka huko.

Aidha machinga machinga hao walisema kuwa wanaiomba serikali ya manispaa ya Iringa kufuata maagizo ya Waziri mkuu ambayo aliyatoa kuhusu namna ya mpangilio mzuri wa wafanyabiashara wadogo wadogo.

Walisema kuwa wamekuwa wanachangia mapato serikalini bila tatizo lakini na kukuza uchumi wa Manispaa nan chi kwa ujumla iwaje ghafla wanataka kuwaondoa kwenye maeneo ambavyo wamezoea kuyafanyia kazi kila siku.

Kwa upande wake katibu wa Machinga Network mkoa wa Iringa Joseph Kilienyi alisema kuwa serikali ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa alisema kuwa wafanyabiashara hao wapo tayari kupangwa kwenye maeneo wanayofanyia baishara na sio kuondolewa kwenye maeneo hayo ambayo wamekuwa wanafanyia baishara kwa miaka mingi bila kusumbuliwa.

Alisema kuwa kuwaondoa machinga kwenye maeneo ambayo wanayafanyia kazi litakuwa jambo gum una haliwezekani hata siku moja hiyo ni lazima serikali ijipange kuhakikisha inatatua jambo hilo kwa kufuata muungozo wa Waziri mkuu.

Kilienyi alisema kuwa anaamini kwenye majadiliano tofauti na kutumia nguvu kama ambavyo baadhi ya viongozi kwenye maeneo mengine wamekuwa wakitumia nguvu kuwaondoa machinga kwenye maeneo ambayo wameyazoea kufanyia kazi biashara zao.

Alisema kuwa wapo tayari kufuata sheria zote za nchi na kuondoka katika maeneo hatarishi kama kwenye mifereji na maeneo mengine kama hayo lakini sio maeneo ambayo wanataka kuwapeleka hivi sasa ambayo kwa kiasi kikubwa sio rafiki na biashara zao.

Kilienyi alisema kuwa wafanyabiasahara wadogo wadogo wamekuwa wanafanya biashara zao katika maeneo hayo kama mbadala wa kuajiliwa na serikali kwa kuwa hivi sasa ajira zimekuwa ngumu kupatika hivyo njia mbadala ni kufanya biashara.

 Alisema kuwa kuwaondoa machika katika maeneo ambayo wamezoea kuyafanyaia kazi ni kupunguza kasi ya kukuza uchumi wananchi na kufifisha maendeleo ya nchi kwa kuwa machinga wamekuwa msaada mkubwa kwa serikali kukuza uchumi wan chi na kuongeza thamani ya mitaji ya matajiri.

Kilienyi alisema kuwa hawapo tayari kuondolewa katika barabara ya mashine tatu bali wapo tayari kupangwa kwenye mpangilio mzuri unaostahili hivyo uongozi wa halamshauri ya Manispaa ya Iringa wanapaswa kufikiri upya kuhusiana na mpango wao. 

Naye mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu aliwataka wafanyabiashara waodogo wadogo kuwa na subira wakati serikali ya halmashauri ya Iringa wakijipanga kuhakikisha wanatatua mgogoro huo na kuwapanga vizuri kwenye eneo hilo la mashine tatu ambalo limekuwa na mzunguko mkubwa wa biashara.

Alisema kuwa machinga wanatakiwa kupangwa kwenye mpangilio mzuri ambao utakuwa rafiki kwao wakati wa kufanya biashara zao.

Msambatavangu aliwataka wamachi kuwa wasafiri na kuondoka mara moja kwenye maeneo hatari ambayo yamekuwa yanaathiri afya zao na mienendo ya biashara zao kwa ujumla.

Alimalizia kwa kusema kuwa serikali ya halmashauri ya wilaya ya Iringa wapo kwenye mjadala wa namna gani wafanyabiashara hao watafanya baishara zao bila kusumbuliwa na mtu yeyote yule.

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment