Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Charles Lengeju akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari nchini na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Huduma na Wanachama wa NHIF Christopher Mapunda akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. |
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anjela Mziray akieleza jambo wakati wa mkutano huo. |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Charles Lengeju kushoto akikambidhi cheti Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Tanga Lulu George kwa kutambua mchango wao klabu za waandishi wa habari hapa nchini.
NA OSCAR ASSENGA, DODOMA
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umesema kwamba wameboresha mifumo ya Tehama ili kuweza kuwasaidia watoa huduma kulipwa madai yao moja kwa moja kutoka Hospitalini kwa lengo la kuondoa ucheleweshwaji wa malipo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Wanachama wa NHIF Christopher Mapunda wakati akiwasilisha mada ya miaka 20 ya mfuko ulipotoka,walipo na wanakoelekea wakati wa mkutano wa waandishi wa habari nchini na NHIF alisema kwa sababu moja ya changamoto kubwa zilikuwa zinaletwa na watoa huduma ni kuchelewa kwa malipo.
Alisema kwa sasa kupitia mfumo huo hakutakuwa na ucheleweshwaji kwa malipo huku akieleza pia hivi sasa wameboresha mifumo ya Tehama na kuwezesha kufanya usajili wa wanachama kupitia mtandao na mwisho kuweza kulipia mchango wake.
Alisema kwa sababu madai yatakuwa yakichakatwa kila siku na mwisho wa siku mfumo umewezesha kulipa madai hayo ndani ya siku 14 tangu kuwasilishwa kwake hivyo watoa huduma watakuwa na kila haja ya kuwahudumia wanachama kwa sababu wanapata fedha zao kwa urahisi zaidi.
Aidha alisema pia mwezi Octoba mwaka huu wataka wanakwenda kufanya kilele cha miaka 20 ya mfuko huo na watazindua Taarifa Appy hivyo wenye simu za smati wataweza kupata taarifa yoyote iwe ni michango, kituo, aina ya dawa kabla ya kwenda kwenye kituo na hivyo kuweza kupunguza malalamiko kwa wanachama.
Awali akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Charles Lengeju alisema hivi sasa mfuko huo umeendelea kufanya maboresho makubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo ulipaji wa madai kwa njia ya mtandao ili kuweza kuepukana na udanyanyifu.
Charles ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Rasilimali Watu na Utawala wa NHIF alisema pia maboresho mengine ni kuwawezesha wananchi mmoja mmoja kujiunga na mfuko huo na kuweza kunufaika na huduma za bima ya afya.
Alisema maboresho mengine ni wameshirikiana na mabenki kuwawezesha wananchi kujiunga na mfuko huo kwa kulipia kwa kudunduliza hatua ambayo wananchi wengine wameweza kunufaika na hivyo kuweza kuondoka na vikwazo vilikuwa vikiwakumba awali.
Aidha alisema pia kuwawezesha wakulima kupitia vyama vya msingi kujiunga na mfuko huo kupitia taasisi za kifedha kuchangia ada zao za uanachama na hivyo kuweza kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapougua.
No comments:
Post a Comment