KASI NDOGO UJENZI BARABARA YA KIDATU - IFAKARA YAMTIBUA PROF. MBARAWA, AMTIMUA MENEJA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 24 September 2021

KASI NDOGO UJENZI BARABARA YA KIDATU - IFAKARA YAMTIBUA PROF. MBARAWA, AMTIMUA MENEJA...!

Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa akimuamuru aliyekuwa Meneja mradi wa ujenzi wa barabara ya Kidatu-Ifakara Km 66.9, Bw. Edan Tesfir kuondoka kwenye eneo la mradi baada ya kushindwa kukidhi matarajio ya Serikali katika ujenzi.

Ujenzi wa nguzo katika daraja la Kilombero ambalo ujenzi wake ni sehemu ya ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara Km 66.9.

Ujenzi wa nguzo katika daraja la Kilombero ambalo ujenzi wake ni sehemu ya ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara Km 66.9.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hanji  Yusuf Godigodi akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa huku mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Abubakar Asenga (katikati), akifuatilia.

Ujenzi wa nguzo katika daraja la Kilombero ambalo ujenzi wake ni sehemu ya ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara Km 66.9.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameelezea kutoridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa Barabara ya Kidatu - Ifakara yenye urefu wa Km 66.9 inayojengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company (RCC), toka Nigeria.

Kufuatia hali hiyo amemuamuru Meneja Mradi wa Ujenzi huo, Bw. Edan Tesfir kuondoka katika eneo la kazi ili kupisha wataalam wengine kufanyakazi.

Ujenzi huo wa barabara kwa kiwango cha lami pia unahusisha madaraja makubwa matano ulianza mwaka 2017 na ulitarajiwa kukamili mwezi Oktoba mwaka huu lakini hadi sasa umefikia asilimia 37.5 hali inayoonesha hautakamilika kwa wakati.

"Tanroads Mkandarasi hana spidi ya kumaliza mradi huu hakikisheni mnazingatia mkataba ili haki itendeke na watakaoshindwa kazi waondolewe, wananchi wanataka barabara," amesema Prof. Mbarawa.

Amesema barabara hiyo ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Dumila Kilosa Mikumi Kidatu Ifakara itaunganisha mkoa wa Morogoro na mikoa ya Njombe na Ruvuma na hivyo kuhuisha uchumi wa mikoa hiyo na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Rudewa-Kilosa Km 24 kuongeza kasi.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro Eng. Baraka Mwambage amesema wamejipanga kuwasimamia kikamilifu wakandarasi mkoani humo ili kuepusha adha kwa wasafiri wakati wa mvua.

Naye Mbunge wa Kilombero, Mhe. Abubakar Asenga amepongeza hatua ya ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na Tanroads na kusisitiza kuwa wananchi wanaisubiri kwa hamu barabara hiyo ili kuhuisha shughuli za kilimo, uvuvi na biashara.

Zaidi ya shilingi bilioni 100 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ambazo ni ufadhili toka nchi za Umoja wa Ulaya, USAID na UKAID.

No comments:

Post a Comment