TCRA YASHIRIKI MBIO ZA MWENGE MAALUM 2021 IPAGALA JIJINI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 29 July 2021

TCRA YASHIRIKI MBIO ZA MWENGE MAALUM 2021 IPAGALA JIJINI DODOMA

 

Afisa Mawasiliano Mwandamizi  wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akiwapa maelezo viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika  Shule ya Msingi Ipangala 'B' iliyopo jijini Dodoma wakati wa mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio hizo isemayo "TEHAMA ni msingi wa wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji"


Baadhi ya viongozi wakipata huduma za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda katika Shule ya Msingi ya Ipagala B jijini Dodoma.


Afisa Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Robin Ulikaye akiwapa elimu wanafunzi  wa shule ya msingi Ipagala B Wakati TCRA ikiwa katika ushiriki wa kutoa elimu katika mbio za Mwenge wa Uhuru jijini Dodoma.


Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mabel Masasi  akikabidhi kitabu cha Mwongozo wa Huduma kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania kwa viongozi wa Mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji"

No comments:

Post a Comment