TANZANIA VINARA KWENYE TAFITI ZA KILIMO AFRIKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 2 July 2021

TANZANIA VINARA KWENYE TAFITI ZA KILIMO AFRIKA

Mkurugenzi Mkuu waTume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akihutubia jana mkoani Morogoro wakati akifungua mkutano wa wadau wa Utafiti nchini.

Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo waTaasisi ya Utafiti ya  Kliniki ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Clinical Research Institute – KCRI ) Prof. Blandina Mmbaga ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho akieleza faida za mpango huo.

Mkurugenzi wa Utafiti, Utratibu wa tafiti na uhamasishaji watafiti kutoka COSTECH Dkt. Bugwesa Katale akiwapitisha wajumbe wa mkutano huo kwenye vipaumbele vya taifa ya utafiti vya 2021/2022 – 2025/2026.

Picha ya pamoja ya wakuu hao wa taasisi zinazojihusisha na kufanya tafiti mbalimbali nchini walioshiriki kwenye mkutano huowa wadau.


Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia na kuchangia mada.

Mkutano ukiendea.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.


Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo 

Mkutano ukiendea.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo 

Mkutano ukiendea.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo 


Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo 

Mkutano ukiendea.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Calvin Gwabara, Morogoro

IMEBAINISHWA kuwa Tanzania bado inaheshimika sana kwenye tafiti afrika hasa za kilimo lakini jitihada zinahitajika katika kuhakikisha kufanya tafiti zinazorandana na mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano ili kupata fedha za kutekeleza.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Utafiti nchini ambao wamekutana kupitia na kuboresha  rasimu ya Muongozo wa vipaumbele vya utafiti vitakavyotelelezwa kwa miaka mitano ijayo kuanzia 2021/2022 hadi 2025/2026.

 " Nchi yetu hivi karibuni imepata miradi mikubwa ya Utafiti ambao mmoja umechukuliwa na Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Gerald Misinzo na Mwingine Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Jijini Arusha hii ni heshima kubwa kama nchi kupata miradi miwili kutoka kwenye mfuko wa Oliver Tambo ambao waliomba watafiti toka nchi nyingi za Afrika lakini tukapata miwili" Alibainisha Dkt. Nungu.

Akizungumzia Mkutano huo wa wadau ambao ni Wakuu wa taasisi zainazoshughulika na kufanya Tafiti amesema kuwa una lengo la kupitia na kuboresha kupitia na kuboresha  rasimu ya Muongozo wa vipaumbele vya utafiti vitakavyotelelezwa kwa miaka mitano ijayo kuanzia 2021/2022 hadi 2025/2026 ili iweze kurandana na Mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano pamoja na Ilani ya Chama tawala (Chama cha Mapinduzi CCM) ambao ilani yao ndiyo inatekelezwa na serikali.

Dkt. Nungu amesema COSTECH kazi yao ni kuratibu tafiti zinazofanyika nchini na kufandhili baadhi ya tafiti hizo kupitia Serikali lakini watafiti wengi wamekuwa wakikosa fedha za utafiti kutoka Serikalini hasa kutokana na tafiti zao kutorandana na Mpango wa Taifa wa Maendeleo na hivyo kutoonekana kuwa na mshiko kwa Wizara ya fedha.

" Sasa tunakutana hapa kuhakikisha kila kipaumbele kichowekwa kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa kinawekewa mikakati ya tafiti ili iwe rahisi kwa watafiti wake kupata fedha za utafiti kutoka Serikalini tofauti na hivyo tutaendelea kukosa fedha kwa kwenda kinyume na vipaumbele vya mpango wa Taifa wa sasa wa miaka mitano 2022/2026," . alisisitiza Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Nungu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti na mafunzo wa Taasisi ya Utafiti ya  Kliniki ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Clinical Research Institute – KCRI ) Prof. Blandina Mmbaga ambaye ni mwenyekiti wa Kikao hicho amesema kupatikana kwa Muongozo mzuri  wa  Utafiti nchini kutasaidia Watafiti wa ndani kuweza kupata fedha badala ya kutegemea fedha za wafadhili pekee.

" Kuna faida kubwa ya serikali kutenga fedha kwaajili ya watafiti wake kufanya tafiti mbalimbali nchini maana watafanya kulingana na mahitaji ya watu wake na nchi kwakuwa fedha za wafadhili zinatoka kwa masharti yao na kufanya tafiti kulingana na maeneo wanayotaka na sio nchi au jamii yetu inavyokata" Alifafanua Prof. Blandina.

Aliongeza kuwa nchi imejiwekea kutoa asilimia moja ya GDP kwenda kusaidia kwenye utafiti nchini lakini haipatikani yote na haitoshi hasa ukizingatia uhitaji mkubwa wa tafiti kwenye kila sekta akitolea mfano Kilimo,Afya, Maji na maeneo mengine.

"Nina matumaini makubwa sasa rasimu hii ya Muongozo wa viapaumbele vya utafiti nchini tunayoifanyia kazi hapa kama wadau itakuwa muongozo mzuri wa watafiti kuandaa maandiko ya utafiti yatakayogusa maeneo hayo ambayo ndio vipaumbele vya Serikali kupitia mpango na kwakuwa tumewashirikisha pia Wizara ya fedha ambao ndio watoa hela naamini kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye maandiko yetu kama watafiti na kuongezeka kwa miradi itakayofadhiliwa na Serikali yetu.

Baada ya kupitia na kuboresha Sera hiyo ya taifa ya utafiti jana katika siku ya kwanza, leo wataangalia sehemu nyingine ya Vigoda vya utafiti yaani Research Chair na namna vinavyoweza kuendeshwa na kufanikiwa kusaidia katika kufanya taifiti nchini kama ilivyo kwenye nchi zingine duniani.

No comments:

Post a Comment