NMB YAZIDI KUWA KARIBU NA WATEJA WAO: DODOMA, SINGIDA NA MANYARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 28 June 2021

NMB YAZIDI KUWA KARIBU NA WATEJA WAO: DODOMA, SINGIDA NA MANYARA

Mkuu wa  Kitengo cha Biashara Benki ya NMB - Alex Mgeni akizungumza na  wafanyabiashara wakubwa wa Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) waliohudhuria jukwaa la NMB Business Executive Network katika hafla iliofanyika katika hoteli ya Morena - Jijini Dodoma.  



Meneja wa NMB Kanda ya Kati – Nsolo Mlozi akizungumza na wafanyabiashara kutoka Singida, Itigi, Ikungi na Manyoni katika mkutano NMB Business Club uliofanyika Mkoani Singida.

Sehemu ya wafanyabiashara walio hudhuria mkutano wa NMB Business Club uliofanyika mkoani Singida.


BENKI ya NMB imeendelea kuwa karibu na wateja wake zaidi ya 700 wa mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kupitia jukwaa la ‘NMB Business Club na ‘NMB Executive network’ kwa nyakati tofauti

NMB imetumia majukwaa hayo kuwakutanisha wateja wao wadogo na wakubwa ili kuwapa elimu ya kuwa wabunifu katika shughuli zao za kujiongezea kipato  ili kukuza biashara zao, lakini pia, wametumia fursa hiyo kuweza kupata maoni kutoka kwa wateja wao  kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo ikiwa ni moja wapo ya njia ya kuwahusisha wateja wao kuwa sehemu  ya ubunifu wa bidhaa zao.


Akizungumza katika NMB Business Club mkoani Singida, Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi aliwahakikishia wafabiashara hao kuwa wapo sehemu salama, kwani NMB iko tayari kukuwa nao katika kila hatua ya shughuli zao. Lakini sio hivyo tu, alibainisha kuwa NMB imeendelea kuwa kinara wa ubunifu wa huduma na bidhaa ili kukidhi matakwa ya wateja wao.


Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB – Alex Mgeni alisema kuwa, kutokana na kukuwa kwa mtaji, NMB imeendelea kuwa benki inayoongoza kwa faida kwa kupata TZS bilioni 206 baada ya kodi ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 45 (YoY), mwaka 2020. Lakini pia wameruhusiwa na TIRA pamoja na BoT kufanya shughuli za Bima ‘bancassurance’ kwa kushirikiana na makampuni 10 ya bima ambapo huduma  inapatikana kupitia matawi yote ya NMB nchi nzima.


Siyo hivyo tu, Alex alibainisha kuwa, NMB imerahisisha ulipaji na ununuaji  kupitia matumizi ya mfumo wa malipo kupitia QR code pamoja na huduma za kibenki kupitia mtandao (Internet banking) na wameingia mkataba na makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Madini (NHIF) kuleta bidhaa ya Dunduliza lengo likiwa kuwawezesha watanzania wote hasa wa vipato vya chini kama wakulima, wachimbaji wadogowadogo  na wajasiriamali kuwa na bima kadiri ya uwezo wao.


Kwa niaba ya wateja, mfanyabishara Neema Mandala aliishukuru NMB kwa kuendelea kuwapa kupaumbele wateja, kwani kupitia majukwaa hayo yameongeza ukaribu wao na benki yao pendwa, lakini pia imekuwa kama njia ya kuwakutanisha wateja na wenzao ili kuendelea kufahamiana zaidi, kitu ambacho kimerahisisha wao kusapotiana kibiashara.


No comments:

Post a Comment