WATANZANIA WANG'ARA MBIO ZA TIGO KILI HALF MARATHON 2021 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 3 March 2021

WATANZANIA WANG'ARA MBIO ZA TIGO KILI HALF MARATHON 2021

Mshindi wa Kwanza Tigo Kili Marathon 2021 upande wa wanawake ni mtanzania anaitwa Failuna Matanga. Fainula Matanga amekamilisha hatua takribani 27,800 idadi ya hatua iliyoweka mkakati wa ONE STEP, ONE TREE na kupelekea Tigo kudhamiria kupanda idaidi ya miti 28,000 kando ya Mlima Kilimanjaro ili kuokoa theluji yake iliyo hatarini kupotea ifikapo 2033. #TigoKiliMarathon2021 #OneStepOneTree























WANARIADHA Wanawake wa Tanzania wameng’ara kwa kuibuka washindi wa Mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon 2021 zilizofanyika mjini Moshi jana jumapili.

Wanariadha hao wazawa wakiongozwa na Failuna Abdi, Angelina Tsere na Anastazia Dolomongo walioshika nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu wameongoza kuanzia nafasi ya kwanza hadi ya kumi.

Failuna Abdi amevunja mwiko kwa mbio hizo ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikitawaliwa na raia wa kigeni na husasani Wakenya ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiibuka washindi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 01:16:17 na kuibuka mshindi wa kishindo, Faiuluina Abdi alisema anayo furaha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake jambo ambalo amekuwa akilitamani. 

“Pamoja na kwamba mbio hizi zimekuwa zikifanyika hapa nyumbani, tumekuwa tukishindwa kuzitendea haki kwa kuwa wageni ndiyo wamekuwa wakizitawala. Ninayofuraha leo nimeweza kulitoa taifa langu kimasomaso,” alisema Abdi.

Katika mbio hizo za Kili Half Marathon mwaka huu, Watanzania wameng’ara sana ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo nafasi ya kwanza hadi ya kumi kwa wanawake imeshikwa na imeshikwa na watanzania huku nafasi ya kwanza kwa upande wa wanaume imeshikwa na Abel Chebet raia wa Uganda aliyetumia muda wa saa 01:03:17 akipishana kwa sekunde moja tu na Mtanzania Gabriel Geay ambaye ametumia muda wa saa 01:03:18 akifuatiwa na Mtanzania mwingine Emmanuel Giniki aliyeshika nafasi ya tatu ambaye ametumua muda wa saa 01:03:31.

Mbio za Kilimanjaro Tigo Half Marathn mwaka huu zimenogeshwa na viongozi m,balimbali walioshiriki mbio hizo akiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira,  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega, na Msanii anayefanya vizuri sana katika sanaa ya vichekesho nchini Tanzania Lucas…. Maarufu kama Joti ambaye ni Balozi wa kampeni ya tigo ya upandaji miti kulinda hifadhi yam lima Kilimanjaro ijulikanayo kama Tigo green For Kili ambayo imezinduliwa mwishoni mwa wiki wilkayani Hai mkoani hapa kwa zoezi la upandaji miti..

Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi zawadi Mkuuu wa Idara ya Tigo Pesa kutoka Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Angelika Pesha alisema kampuni yake inayofuraha kuchangia maendeleo ya michezo nchini na hususani riadha ambayo pia huboresha afya.

Pesha alisema Tigo imekuwa mdhamini wa mbio za Kili half Marathon kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo na kuongeza kuwa itaendelea kudhamini pamoja na kuboresha mbio hizo kila mwaka.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega aliishukuru Tigo kwa kudhamini mbio hizo na kuwataka wakazi wa Moshi kutumia fursa zitokanazo na mbio hizo kujijenga kiuchumi.

 

“Mbio hizi zimeleta wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 hapa mjini Moshi. Idadi hii kubwa ya watu itokanayo na mbio hizi ni fursa nzuri ya kibiashara na ni vyema wakazi wa Moshi wakaichangamkia,” alisema Waziri Ulega.

Mbio za Kilimanjaro Marathon hufanyika mjini Moshi kila mwaka. Idadi ya washiriki wa mbio hizo imekuwa ikiongezeka kwa mujibu wa waandaaji kutoka wakimbiaji 750 wakati za kikianza hadi kufikia washiriki 11,000 kwa sasa.

 

No comments:

Post a Comment