WAZIRI MKENDA AVIPONGEZA VIWANDA VYA SUKARI TPC MOSHI NA MANYARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 3 March 2021

WAZIRI MKENDA AVIPONGEZA VIWANDA VYA SUKARI TPC MOSHI NA MANYARA

 

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizuru kukagua kiwanda cha sukari cha Manyara kilichopo Wilaya ya Babati jana ambapo amekipongeza kwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji na kusaidia wakulima wadogo kupata soko la uhakika la miwa.



Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiongea watumishi na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Manyara ambapo amekipongeza kwa kuweza kuzalisha tani 8,133 mwaka 2021 toka tani2,700 mwaka 2015/16  za sukari huku kikinunua miwa yote ya wakulima .Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange na Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Bi.Mwamini Juma.



Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na menejimenti ya kiwanda cha sukari TPC cha Moshi jana ambapo amekipongeza kwa kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji na matumizi ya mbegu bora hali iyosaidia kuongeza tija na uzalishaji sukari toka tani 88,968,000 mwaka 2019/20 hadi tani 101,403 mwaka 2021 huku ikilipa gawio serikalini la shilingi Bilioni 15 mwaka 2021 tofauti na viwanda vingine vikubwa vya sukari.

No comments:

Post a Comment