MAREKANI na washirika wake wanapaswa kukataa miito ya dunia inayopiga marufuku mifumo ya silaha za intelijensia bandia, zinazojiendesha, kulingana ripoti rasmi iliyoitishwa kwa ajili ya Rais wa Marekani na baraza la Congress.
Inasema kuwa intelijensia bandia ita "fupisha muda wa uchukuzi wa maamuzi " na inahitaji mashambulio ya kijeshi ambayo mwanadamu hawezi kuyajibu haraka vya kutosha peke yake.
Na imeonya kuwa Urusi na Uchina zina uwezekano mkubwa wa kutotekeleza aina yoyote ya mkataba wa aina hiyo.
Lakini wakosoaji wanadai kuwa mapendekezo hayo yanaleta hatari ya kusababisha mashindano ya silaha "yasiyo ya uwajibikaji ".
"Hii ni ripoti ya inashitua nakuogofya ambayo inaweza kusababisha maamuzi ya utengenezaji wa silaha za intelijensia kufanya maamuzi ya nani wa kumuua," alisema Profesa Noel Sharkey, msmaji wa kampeni ya kuzuia roboti zinazoua.
" Mwanasayansi wa ngazi ya juu zaidi katika sayari dunai ameowaonya kuhusu athari, lakini bado wanaendelea.
"Hii itasababisha ukiukaji mbaya wa sheria za kimataifa ."
Ripoti hiyo inasema kuwa kama mifumo ya silaha zinazojiendesha itajaribiwa ipasaavyo na kuidhinishwa kwa ajili ya kutumiwa na binasamu, basi hii inapaswa kufuata sheria za kimataifa za kibinadamu.
Mapendekezo yalitolewa na Kamati ya taifa ya Usalama kuhusu intelijensia bandia- taasisi ambayo iliongozwa na mkuu wa zamani wa Google Eric Schmidt na Naibu waziri wa zamani wa usalama, Robert Work, ambaye alihudumu katika utawala wa marais Obama na Trump.
Wajumbe wengine ni pamoja na Andy Jassy, mkurugenzi mkuu ajaye wa Amazon, Mkuu wa intelijensia bandi wa Google na Microsoft Dkt Andrew Moore na DktEric Horvitz, na Mkuruhgenzi mkuu wa kampuni ya Oracle, Safra Catz.
Sehemu kubwa ya ripoti hiyo yenye kurasa 750-iliangazia zaidi juu ya jinsi ya kukabiliana na nia ya Uchina ya kuwa namba moja duniani katika Intelijensia bandia ifikapo mwaka 2030.
Inasema kuwa viongozi wa ngazi ya juu wa kijeshi wameonya kuwa Marekani inaweza "Kupoteza ukuu wake wa mbinu zake za kijeshi katika miaka ijayo" kama Uchina itaidhinisha mifumo ya silaha hizo znazojiendesha AI-haraka zaidi -kwa mfano kwa kutumia mashambulio ya kundi la ndege zisizo na rubani kushambulia jeshi la majini la Marekani.
"Wizara ya Usalama imekuwa ikitumia vifaa vya meli, ndege, na vifaru na sasa inajaribu kutumia kompyuta ," ripoti hiyo inasema.
"Kama vikosi vyetu havijapewa mifumo ya Intelijensia bandia AI-inayoongozwa na dhana ambazo zinazidi za wale wanaowapinga litakuwa ni tatizo katika vita."
Ripoti hiyo inabashiri kuwa silaha za Intelijensia zitabadili "masuala yote yanayohusu jeshi ", na mazungumzo kuhusu kukabiliana na siku zijazo.
No comments:
Post a Comment