RAILA ODINGA AISHINDA CORONA, ATOKA HOSPITALI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 15 March 2021

RAILA ODINGA AISHINDA CORONA, ATOKA HOSPITALI...!

Raila Odinga

KIONGOZI wa Chama cha ODM nchini, Kenya Raila Odinga ametoka hospitalini na sasa anaendelea kupata afueni nyumbani kwake Karen mjini Nairobi.

Raila Odinga alituma video kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akifanya mazoezi ya viungo, huku akiwa anasema "Nafurahi nimerejea nyumbani,".

Raila alisema kwamba amethibitishwa kupatikana na virusi vya corona Alhamisi, na kusihi raia kuendeleza kanuni za kukabiliana na virusi hivyo.

Raila mwenye umri wa miaka 76 alithibitisha kwamba amefanyiwa msururu wa vipimo katika hospitali ya Nairobi Hospital baada ya kulalamika kwamba ana uchovu aliporejea Nairobi kutoka kampeini za siku tano katika eneo la Pwani kufanyia kampeni ripoti ya BBI.

"Ingawaje vipimo vilikuwa vingi, matokeo ya uchunguzi mmoja muhimu yamekuwa wazi na nimewaruhusu madaktari wangu kutangaza kwa umma kwamba nina virusi vya Covid-19", alisema waziri huyo mkuu wa zamani.

Kiongozi huyo wa chama cha (ODM) amekuwa akipata matibabu katika hospitali ya Nairobi Hospital.

Daktari wa Raila Dkt. David Oluoch Olunya, Alhamisi alisema kuwa kiongozi huyo wa ODM anapokea matibabu na wanazidi kuifuatilia kwa makini hali yake.

Wakati akiwa anaendelea kupata matibabu, Raila Odinga aliwashukuru Wakenya kupitia mtandao wa Twitter kwa kumuunga mkono:

"Wakenya wenzangu, Thank you for the overwhelming messages of goodwill. I'm feeling much, much, better now and following doctors' orders. Asanteni!".

-BBC

No comments:

Post a Comment